MWANADIPLOMASIA ya Shahada ya Juu ambaye pia ni Naibu Katibu wa Baraza la Wazee Kata ya Kijichi mkoani Dar es Salaam Juliana Lubuva amempongeza Rais Samia Suluha Hassan kwa hatua yake ya kukutana na wazee na kupata fursa ya kuzungumzia mambo mbalimbali yanayohusu ujenzi wa taifa.
Amesema alichokifanya Rais Samia ni kitu kizuri kwani kitendo cha kukaa pamoja na wazee na kujadiliana baadhi ya mambo ni hatua kubwa na ya mfano kabisa na kikubwa amekuwa muwazi katika yale anayoyaamini kwenye serikali yake.
Akizungumzia kikao hicho cha Rais na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa niaba ya wazee wote nchini, Mwanadiplomasia huyo amesema Rais Samia amefanya jambo kubwa na lakupongezwa, ametumia kikao hicho kufafanua mengi kuhusu mstakabali wa wazee nchini.
"Rais Samia ametutendea haki wazee wa Dar Es Salaam kwaniaba ya wengine hapa nchini kwani hata katika hotuba yake unaona kabisa kwamba anachokiongea kinatoka moyoni kwake na si vinginevyo," amesema Juliana Lubuva.
Ameongeza kwamba "kuna haja kama taifa kurudi kwenye maadili kwani hivi sasa maadili yameporomoka sana na ndio maana leo hii kijana hawezi kumpisha Mzee kwenye vyombo vya usafiri jambo ambalo huko nyuma halikuwepo."
Aidha Juliana amemuelezea Rais Samia kama mwanamama jasiri na mwenye mitazamo chanya Kwa nchi yake na watu wake na ndio maana amekuwa mkweli hata kuelekea mabadiliko ambayo ametangaza kuyafanya ndani ya Serikali yake.
Amefafanua katika kikao hicho wazee walikuwa na mahitaji yao ambayo wanataka watimiziwe ikiwa pamoja na asilimia 10 zinazotokana na mapato ya Halmashauri na wao waweze kufikiriwa kwani ni sehemu ya kundi maalum .
Pia uwakilishi kwenye vyombo vya maamuzi kama vile Bunge na mamlaka zingine ili na wao waweze kuwa na mtu wakuwasemea changamoto zao, lakini pia kwenye sekta ya afya wamesema bado hakujakuwa rafiki sana Kwa upande wao.
"Kiukweli Rais Samia ameonesha kukubaliana na hoja karibu zote za wazee huku akihaidi kuzifanyia kazi siku za mbeleni na zingine tumemsikia akimwagiza Waziri wa afya kushughulikia haraka hususani kero zinazohusu afya,"amesema Juliana.
Amesema kingine kilichomvutia ni jinsi Rais alivyokuwa muazi ambapo amewaeleza wazee kuwa tayari na kuyapokea mabadiliko ambayo atayafanya siku si nyingi huku akisema anajua kuwa watoto wao wapo.lakini waweze wavumilivu.
Hata hivyo amesema Rais Samia amewaeleza kutokana na utekelezaji wa miradi mikubwa katika nchi ndio maana hata suala la kupandisha mishahara litafanywa hapo baadae huku akisisitiza kumaliza miradi yote ya kimkakati.
Juliana Lubuva ambaye ni Mwanadiplomasia ya Shahada ya Juu ambaye pia ni Naibu Katibu Baraza la Wazee Kata ya Kijiji akifuatilia kikao kati ya Rais Samia na Wazee Mkoa wa Dar es Salaam
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment