MISS MWANZA HATARI WAPANIA KUBAKIA TENA NA TAJI 2021 | Tarimo Blog

 

   Na.Khadija Seif, Michuzi Tv

PAZIA la Kusaka Mrembo atakae iwakilisha Kanda ya ziwa yafunguliwa rasmi.       

Akizungumza na Michuzi Tv Muandaaji wa Shindano Hilo kwa upande wa Mwanza Phinnley Ngeta amesema kwa Sasa wamefungua rasmi Shindano Hilo na wapo tayari kupata warembo wataokidhi vigezo vya kushiriki Miss Mwanza na hatimae kuwania Taji la Miss Tanzania.                

"Tumefunga rasmi Shindano la Miss Mwanza na tunategemea kupata Warembo wazuri wasomi bila kusahau wenye vipaji vingi,hivyo nitamke rasmi na kuwakaribisha warembo kuchukua fomu ili kushiriki kikamilifu."        

 Hata hivyo Ngeta amesema wanatarajia Kufanya usahili mwishoni mwa mwezi May 29 mwaka huu ili kufanya mchujo wa Kwanza na kupata Washiriki watakaoweza kuingia kambini.  

"Tutegemee kupata Mrembo atakaeweza kuiwakilisha vizuri Kanda ya ziwa na ikumbukwe tu Miss Tanzania 2019  Sylivia bebwa alitokea Kanda ya ziwa hivyo tutegemee Tena Taji hilo kubakia Mwanza kwa Mara nyingine tena na Mrembo alikua na nidhamu Sana kiasi Kwamba mpaka Leo ameweza kukaa na Taji Hilo bila purukushani yoyote kuanzia kwenye jamii mpaka kwenye mitandao"             

 Pia amewaomba Wadau wa urembo kujitokeza Kudhamini Shindano Hilo  ili kufanikisha Mchakato mzima.

"Kufanya Shindano Kama hili sio tu kwa ajili ya Warembo tu bali ni Mojawapo ya njia nzuri ya kutangaza vivutio vya Utalii na Kwa Kanda ya ziwa tumebarikiwa vitu vingi ikiwemo vyakula aina ya Samaki Sato kutoka ziwani na vitu vingi."


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2