Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa Mteule wa Singida, Dkt. Binilith Mahenge akiungana na Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti katika Kata ya Zuzu uliofanyika katika shule ya Sekondari ya Zuzu.
Paroko Pinoy Thomas wa Kanisa Katoliki Nzinje, Zuzu akipanda mti wakati wa kampeni hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Benki ya Exim, Stanley Kafu akishiriki kupanda miti wakati wa kampeni hiyo. Upandaji miti unaoratibiwa na Taasisi ya Habari Development (HDA) umefadhiliwa na benki hiyo.
Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Pinda, Maccelina Chuwa akipanda mti.
Wadau mbalimbali wa mazingira wakipanda miti eneo la shule ya Sekondari Zuzu.
Wanafunzi wa shule ya Zuzu wakishiriki kupanda miti
Kikundi cha ngoma cha Mwino kikitumbuiza
Katibu wa Taasisi ya Habari Development (HDA), Bernard James akielezea umuhimu wa kupanda miti na kuifanya Dodoma ya kijani, lakini pia aliishukuru Benki ya Exim kufadhili kampeni hiyo ya upandaji miti.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Benki ya Exim, Stanley Kafu akizungumza wakati wa kampeni hiyo na kuahidi kusaidia uchimbaji wa kisima cha maji ya kumwagilia miti hiyo pamoja na matumizi mengine ya binadamu.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Mahenge akiwa na Waziri Mkuu mstaafu, Mzee PindaKatibu wa Taasisi ya Habari Development (HDA), Bernard James akielezea umuhimu wa kupanda miti na kuifanya Dodoma ya kijani, lakini pia aliishukuru Benki ya Exim kufadhili kampeni hiyo ya upandaji miti.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Benki ya Exim, Stanley Kafu akizungumza wakati wa kampeni hiyo na kuahidi kusaidia uchimbaji wa kisima cha maji ya kumwagilia miti hiyo pamoja na matumizi mengine ya binadamu.
Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti na kuwataka wananchi kushiriki kwa ukamilifu kupanda miti na kuitunza.
Wanafunzi wakibeba mbolea ya kupandia miti
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge na Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda wakiwa na kikosi cha Taasisi ya Habari Development baada uzinduzi wa kampeni hiyo.
Mdau nakuomba uendelee kusikiliza/kuona kupitia clip hii ya video yaliyojiri wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo....
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment