Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk Amos Nungu akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuelekea Wiki ya Ubunifu itakayoanza kesho, Mei 17 jijini Dar es Salaam na kumalizika Mei 22, 2021.
Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Maendeleo ya Watu (HDIF), Joseph Manirakiza akizungumza katika mkutano huo wa kuelekea wiki ya Ubunifu inayotarajiwa kuanza kesho jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Ukuaji wa Uchumi Shirikishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Emmanuel Nko akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wao kuelekea wiki ya ubunifu inayoanza kesho Mei 17, hadi Mei 22, 2021 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Maendeleo ya Watu (HDIF), Joseph Manirakiza akizungumza na waandishi wa habari wa katika kuelekea wiki ya Ubunifu inayotarajiwa kuanza kesho jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk Amos Nungu akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuelekea Wiki ya Ubunifu itakayoanza kesho, Mei 17 jijini Dar es Salaam na kumalizika Mei 22, 2021.
KATIKA kuhakikisha asilimia 80 ya wananchi wote nchini wanapata huduma za mtandao ifikapo mwaka 2025, serikali imedhamiria kuanzisha kiwanda cha kuzalisha simu janja ( smart phones), nchini kutimiza azma yake hiyo.
Uanzishwaji wa kiwanda hicho cha simu utaenda sambamba na upanuzi wa upatikanaji wa mkondo wa Taifa ili kuunganisha maeneo mengi yenye makazi ya watu yasiyofikiwa na kampuni za simu.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt Amos Nungu ameyasema wiki hii wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuelekea Wiki ya Ubunifu itakayoanza kesho, Mei 17 jijini Dar es Salaam na kumalizika Mei 22, 2021.
Wiki hiyo ya Ubunifu nchini imeandaliwa na Mfuko wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Binadamu (HDIF) kwa kushirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia ( COSTECH) pamoja na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP).
Amesema kauli mbiu ya wiki ya Ubunifu mwaka huu ni Uchumi wa Kidijitali Stahimilivu na Jumuishi, ambapo ili kufikia malengo hayo serikali iliamua kuanzisha Wizara inayoshughulikia masuala ya Tehama ili kila mtu aweze kufikiwa na huduma hizo.
Ameelez kuwa, hivi karibuni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitangaza zabuni kwa wadau mbalimbali watakaoweza kuanzisha kiwanda cha kuzalishia simu janja ili simu hizo ziweze kupatikana kwa bei nafuu na kuongeza ajira.
Dkt. Nungu amesema serikali imeweka sera ya kuwatambua wabunifu mbalimbali nchini kwani hata kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imewataka wananchi wote wafikiwe na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Aidha Dkt. Nungu amesema, wamejifunza mambo mengi baada ya kutokea kwa ugonjwa wa corona nchini ambapo baadhi ya shughuli zililazimika kusimama na wanafunzi wengi walioko vijijini walishindwa kuendelea na masomo kutokana na kutokuwepo kwa teknolojia ikiwemo ya kidijitali tofauti na wa mijini ambapo wanafunzi waliendelea kusoma kupitia mitandao
Amesema kuwa njia pekee ya kujiandaa na majanga kama hayo ni lazima kuwepo bunifu mbalimbali zitakazotatua changamoto kwenye jamii na hiyo itasaidia kubaki na uchumi imara.
"Tunajipanga ili kuhakikisha miaka ijayo Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi na Teknolojia ya Ubunifu (MAKISATU), yanafanyika kuanzia ngazi ya Wilaya hadi Taifa kuibua wabunifu ili waonekane na wafadhili ili kuwaendeleza," alisisitiza.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Maendeleo ya Watu (HDIF), Joseph Manirakiza amesema kwa miaka saba tangu kuanzishwa kwa wiki hiyo, wameweza kufika zaidi ya Mikoa tisa na sasa serikali imeona ni muhimu kuweka sera za kukuza ubunifu nchi nzima.
Amesema dhumuni kubwa la wiki ya ubunifu ni kuto nafasi kwa wavumbuzi, wabunifu, watunga sera, wafadhili, watafiti na wadau wengine katika mfumo wa ubunifu, kubadirishana mawazo kuhamasisha, kujenga ushirikiano na mambo mengine kadhaa ikiwemo mijadala ya kisera yenye lengo la kuboresha mazingira ya ubunifu nchini.
Pia amesema uwepo wa mifumo thabiti ya teknolojia itasaidia kuweka uchumi stahimilivu na kutoacha wananchi nyuma hasa waishio vijijini.
Naye, Mkuu wa Kitengo cha Ukuaji wa Uchumi Shirikishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Emmanuel Nko amesema ubunifu ni nyenzo mojawapo ya kufanikisha maendeleo kwa kasi na kuongeza ajira kwa wananchi wengi nchini hususani Vijana.
Amesema wiki ya ubunifu ni jukwaa huru linalowapa nafasi vijana kuonesha bunifu zao, kukutana na wadau, wafadhili na wanunuzi.
"Ubunifu umetoa ajira kwa vijana wengi kwani wamekuwa wakitumia teknolojia kutangaza biashara zao na kuziongezea thamani. Changamoto zipo ikiwemo sheria lakini kupitia jukwaa hili tutajua nini cha kufanya kuzirekebisha." Amesema Nko.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment