RAIS DK.MWINYI AJUMUIKA NA WANANCHI WA MKOA WA KUSINI UNGUJA KATIKA FUTARI ALIYOWAANDALIA UNGUJA | Tarimo Blog

 


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja katika Sala ya Magharibi, ikiongozwa na Sheikh.Said Abubakar, iliofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein (SUZA) Tunguu Wilaya ya Kati Unguja,  wakati wa hafla ya Futari Maalum aliyowaandalia Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Sheikh Muazi Jongo Hassan, baada ya kumaliza kwa  Sala ya Magharibi iliofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein (SUZA) Tunguu Wilaya ya Kati Unguja na (kulia kwa Rais)Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi) na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe Rashid Hadidi Rashid.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk., Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja katika Futari Maalum aliyowaandalia Wananchi wa Mkoa huo iliofanyika  katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein (SUZA) Tunguu Wilaya ya Kati Unguja (kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba na Sheria Utumishi na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman.

WANANCHI wa Mkoa wa Kusini Unguja wakipata futari katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein (SUZA) Tunguu Wilaya ya Kati Unguja ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi, kwa Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja.(Picha na Ikulu)


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2