RC KUNENGE ATOA SALAMU ZA WAKAZI WA MKOA WA DAR ES SALAAM KWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN | Tarimo Blog
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Abubakar Kunenge ametoa salamu za wakazi wa Mkoa huo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambapo amesema wakazi hao wanampenda na waamuunga mkono wakati wote.
Akizungumza leo wakati akitoa salamu za mkoa huo,Kunenge amesema kwamba wakazi wa mkoa huo wanamkaribisha na kwamba Dar es Salaam iko shwari, iko salama na kwamba wanampenda sana na wanamuahidi kutomuangusha.
"Tukio hili unalofanya hapa la kuzungumza na wazee wa Dar es Salaam ni tukio adhimu na ni tukio la kihistoria, watangulizi wako kaunzia awamu ya kwanza hadi awamu ya Tano walikuwa na utaratibu huu wanapokuwa na masuala muhimu, masuala mazito au wanapoona wanahitaji kuzungumza a kubadilisha mawazo na wazee.
"Kwetu sisi utaratibu huu ni utamaduni mzuri, tunafanya hivi kwasababu wazee wamekuwa wakitumika kutoa miongozo na ushauri mbalimbali , wazee ni hazina na tunu kwa Taifa, maoni yao, ushauri wao umekuwa ukisaidia taifa letu, hivyo umefanya vizuri kuzungumza nao na tunaamini hata wao wataondoka na furaha.
"Rais leo ulituagiza kwamba ulipenda kuzungumza na wazee hawa, sisi wasaidizi wako tulifanya maandalizi na tulitajaria wawepo wazee 900 lakini kwa mapenzi mema waliyonayo kwako tunao wazee 1100 ambao wako hapa.
"Waze hawa wanapenzi makubwa sana na wewe, pamoja na tulisema waje tu wale ambao wenye mialiko, lakini wamekuja hata wale ambao hawana mialiko, hivyo tumeona ni vema tukabanana ilimradi wakuone,"amesema Kunenge.
Amefafanua hiyo ni idadi ndogo kwa wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam na hawa wazee wanawakilisha wazee walioko kwenye maeneo mbalimbali ya nchi yetu."Hivyo katika kuleta uwiano sawa, kwa wazee hawa wa Dar es Salaam wametoka maeneo mbalimbali.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment