TIGO WAWAKUMBUKA YATIMA BUKOBA. | Tarimo Blog
Pichani Ni Watoto Yatima wa Kito cha UYACHO wakiendelea kufurahia Futari waliyoandaliwa na Tigo.
Sehemu ya Watoto wa Kituo Cha kulelea Watoto Yatima cha UYACHO wakipokea chakula (Iftari) kilichoandaliwa na Kampuni ya Tigo kwa ajili yao.Sheikh wa Wilaya ya Bukoba Mjini Yusufu Habib Kakwekwe akiongoza safu ya Viongozi na waalikwa kwenye meza ya chakula wakati wa Hafla ya Futari ya pamoja na Watoto Yatima
Sehemu ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Mawasiliano Tigo, katika Picha ya pamoja wakati wa Hafla ya Futari kwa Watoto Yatima wa UYACHO Bukoba.
Na Abdullatif Yunus Michuzi TV.
Tukiwa tunaelekea ukingoni mwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Kampuni ya Mawasiliano ya Mtandao wa Tigo, Mkoa Kagera wameshiriki Futari ya pamoja na Watoto Yatima wanaolelewa katika Kituo cha Watoto Yatima cha UYACHO.
Kituo hiki kilichopo Kata Hamugembe Manispaa ya Bukoba kimekuwa kikipokea na kulea Watoto tangu Mwaka 1999, kikiendeshwa kwa Hisani za mashirika, Taasisi, watu na misaada mbalimbali, ambapo kwa Sasa Kituo hiki kina jumla ya Watoto 72, huku wengi wao wakiwa wamepitia Kituo hicho, na Sasa wapo katika nafasi nzuri kimaisha.
Akitoa neno la shukrani kwa Niaba ya Bi Saada Kijana wake Sadath Kachwamba, ameipongeza Kampuni ya Tigo kwa kufikiria kushiriki na Watoto Yatima hao, licha ya Fadhila na Thawabu kubwa kiimani wanazopata kutokana na tendo hilo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment