Na Woinde Shizza, Michuzi Tv-Arusha
WANANCHI ambao ni wakulima wa mazao mbalimbali hapa nchini wametakiwa kujijengea tabia ya kupima udongo katika mashamba yao ili wanapolima walime kilimo cha uhakika cha kupata mazao mengi yenye tija .
Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa kampuni inayiojishughulisha na upimaji wa udongo kwa wakulima wakubwa,wakati na wadogo (LSSL) Dkt Edmond Matafu wakati akitoa elimu kwa wakulima wa zao la parachichi walioko katika kijiji cha Ngyani wilayani Arumeru mkoani Arusha ambapo alisema kuwa ni vyema mkulima wa zao lolote lilile akapima aridhi yake kabla ya kuotesha kitu chochote.
Alisema kuwa upimaji wa udongo katika shamba unalotaka kulima unasaidia mambo mengi sana ikiwemo kujua ni aina gani ya udongo uliopo katika eneo husika ,ni aina gazi ya zao ambalo linaweza kustawi katika udongo huo ,udongo huo unahitaji mbolea au hauitaji pamoja na kujua aina ya mazao yanayofaa katika shamba la mkulima, kujua virutubishi vilivyopo katika udongo na ni kwa kiasi gani, pamoja na mkulima kununua mbolea kulingana na upungufu wa virutubishi vinavyohitajika kwenye udongo. .
Alisema kuwa wakulima wengi wamekuwa wanalima mazao mbalimbali bila kupima udongo wa eneo husika hali ambayo inawasabishia kukosa mazao mengi na wakati mungine kukosa kabisa mazao,ambapo alibainisha kuwa bado wakulima wengi hawana uelewa juu ya afya ya udongo ambayo ndio msingi mkubwa wa kilimo.
“kuna wakulima wamekuwa wakitaka kulima kilimo cha biashara lakini unakuta wamejijengea tabia ya kuzani kuwa ukilima kukiwa na maji basi wamemaliza na wamepata jambo ambalo si lakweli ukitaka kulima kilimo cha biashara na upate faida na mazao mengi kwanza kunatakiwa kupima udongo wako na kuujua ukisha upima ndio unanze kulima apo utakuwa umelima kilimo cha uhakika na utapata mazao ya uhakika “alifafanua Matafu
Alisema ni vyema maafisa ugani wakaendelea kutoa elimu zaidi kwa wakulima kwani bado elimu hii bado haijawafikia wakulima walio wengi hali inayopelekea kutokuona umuhimu wa kupima udongo na kuendelea kulima kilimo cha mazoea kisichokiwa na tija.
Kwa upande wake mtaalamu wa upimaji udongo wa kampuni hiyio Haji Salum alisema kuwa elimu ikitolewa zaidi kwa wakulima itasaidia kutunza mazingira kwasababu baadhi ya virutubishi vikizidi kwenye udongo huweza kuharibu mazingira na kufanya mimea ya aina yoyote isiweze kuota ambapo mkulima atakapo pima udongo katika shamba lake atajua mahitaji ya mbolea au virutubisho vinavyohitajika na kujua jinsi ya kuboresha udongo huo.
Alieleza kuwa lengo la kuhamasisha upimaji wa udongo ni ili kuwasaidia wakulima wote nchini kujua afya ya udongo hasa tindikali (pH), kujua virutubishi vilivupo katika udongo kabla ya kulima zao lolote na kuwezesha kujua kiasi cha mbolea inayojitajika katika mmea.
“Kwa kupima udongo mkulima atajua virutubishi vilivyoko kwenye udongo Kama vile, Naitrojen, Fosiforasi, Potasiamu, Salfa pamoja na virutubisho vidogo vidogo ambavyo ni muhimu kwa ukuaji na uzalishaji wa mmea Kama vile boron, zinc, copper, na kuendelea,” Alieleza Haji
Alifafanua kuwa ni muhimu kwa wakulima kabla ya kulima au kuotesha kujua kujua afya ya udongo wa shamba lake ili kuweza kufanya kilimo chenye tija ambapo anatakiwa kuchukua sampuli ya udongo kwa njia ya kupishanisha (zigzag)na kupeleka katika maabara ili kujua aina ya mbolea na mazao yanayokubali katika eneo hilo.
“Majibu mazuri ya udongo yanatokana na umakini wa uchukuaji wa sampuli katika shamba ambapo anayechukua udongo anatakiwa kuchima vishimo zaidi ya 15 vyenye kina Kati ya sentimita 15 hadi 20 na kukusanya sapuli hizo toka maeneo mbalimbali ya shama analotarajia kulima,”alifafanua.
Aliendelea kusema kuwa baada ya kukamilika kwa zoezi la ukusanyaji wa sampuli, udongo huo utapelekwa katika maabara ambapo majibu yake yatatoka baada ya siku kaadhaa lakini pia kina kifaa cha kupima udongo papo kwa hapo.
“LSSL tuna aina mbili za teknolojia za kupima udongo moja ya papo kwa hapo na nyingine ni ya maabara ambapo hii ndio inayotoa majibu mengi zaidi ikiwa ambayo Ni pamoja na aina ya mazao yanayofaa katika shamba lakini Kuna maeneo mengine pia majibu yanatoka kuwa hapafai kulima zao lolote na hapa panahitajika jitihada za kurutubisha udongo,” Alisema Haji
“Kuna madhara unapoweka mbolea mahalo pasipo hitaji mojawapo ikiwa ni kuharibu udongo na kupunguza uzalishaji wa mazao na sisi LSSL tunapima udongo ili kusaidia wakulima kuongeza tija ya mazao wanayozalisha,”alibainisha.
Alieleza ikumbukwe kuwa udongo ndio msingi wa kilimo hivyo wakulima wawekeze kwenye afya ya udongo ili waweze kulima kilimo Bora chenye manufaa kwao na kwa taifa zima.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment