BILIONEA LAIZER AIOMBA SERIKALI KUONGEZA IDADI YA WALIMU KATIKA SHULE ALIYOIJENGA | Tarimo Blog

Bilionea Saniniu Laizer akizungumza na waandishi wa habari( hawapo pichani) wakati akielezea maendeleo ya shule aliyoijenga kwa fedha zake na kisha kuikabidhi kwa Serikali wilayani Simanjiro.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Swedefrida Msoma akifafanua jambo.
Sehemu ya wanafunzi wa kabila la Wamasai wakiwa katika Shule ya Saniniu Laizer ambayo imejengwa na Bilionea Saniniu Laizer.

 Na Mwadishi Wetu, Manyara 

BILIONEA Saniniu Laizer ametoa ombi kwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kuongeza walimu katika shule ya Saniniu Laizer iliyopo katika Kijiji cha Naepo Kata ya Naisinyai  wilayani Simanjiro mkoani Manyara.

Shule hiyo inayofundisha kwa lugha ya Kingereza ambayo imejengwa na Bilionea Laizer lengo lake ni ni kusaidia watoto wa jamii na tangu ilipoanza muitikio umekuwa mkubwa kwani hivi sasa inajumla ya wanafunzi 293 lakini walimu waliopo ni wawili tu, hivyo ameiomba Serikali kuongeza walimu shuleni hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari ambao walifika kuangalia maendeleo ya shule hiyo,Bilionea Laizer ameonesha kufurahishwa kwake na idadi ya wanafunzi ambao wapo shuleni hapo lakini akatumia nafasi hiyo kuelezea changamoto waliyonayo ni uhaba wa walimu.

"Changamoto ambayo tunayo kwa sasa katika shule hii ni uhaba wa walimu, waliopo ni wawili tu na wanafunzi waliopo ni 293, hivyo tunaiomba Serikali yetu kuangalia namna ya kutusaidia kuongeza walimu ili kufundisha watoto hawa.

"Aidha tunatoa ombi kwa Serikali itusaidie kwenye ujenzi wa mabweni katika shule hii,"amesema Bilionea huyo ambaye ameamua kuweka mkazo katika elimu kwa watoto wa jamii ya wafugaji.

Katika hatua nyingine Bilionea huyo ametumia nafasi hiyo kueleza wakati umefika kwa wachimbaji wadogo wadogo wa Manyara kuona umuhimu wa kuleta maendeleo katika mkoa wao kwani wanapata fedha nyingi kutokana na uchimbaji madin, hivyo waguswe kusaidia jamii ya Kimasai hasa ka kuhakikisha inapata elimu.

Akielezea zaidi amesema uwepo wa shule hiyo umewezesha kufungua wigo hadi watu wazima wa jamii ya Kimasai wamekuwa wakienda kupata elimu ambapo wametengewa muda wa saa tatu."Hawa watu huko nyuma walikosa elimu lakini kwa kutambua umuhimu wake na baada ya kujenga shule hii wameamua kuja kuifuata hapa."

Aidha amesema wanampango wa kujenga bwalo kwa ajili ya kulia chakula na wako kwenye maandalizi, tayari wameshaleta tofali ili kuanza ujenzi ambapo pia watajenga mabweni kwa ajili ya wanafunzi wanaotoka mbali na shule hiyo.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Swedefrida Msoma amesema mpaka sasa muitikio ni mkubwa kwani wameandikisha wanafunzi Sana na wameweza kuandikisha zaidi ya wanafunzi miambili na tisini na tatu (293)  amesema J293 wa jamii ya kabila la Kimasai."Jamii hii ya Kimasai wanaakili sana , tumewafundisha muda mfupi lakini wameweza kuelewa."

Amefafanua awali kulikuwa na ugumu kwasababu ya mawasiliano kwani lugha ambayo walikuwa wamezoea kuitumia ni Kimasai lakini sasa wanaongea Kiswahili na Kingereza.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2