AWESO AWAANDAA WAHANDISI WA MAJI KIMKAKATI KWENDA KUIFANYA KAZI BAADA YA KUONGEZEWA FEDHA | Tarimo Blog

WAZIRI WA MAJI Mh. Jumaa Aweso amewasihi wahandisi wa Maji nchini kujidhatiti na kuwa tayari kuifanya kazi kubwa ya utekelezaji wa Miradi ya Maji ambapo kutokana na mageuzi yanayoendelea sekta ya Maji, Wizara imeaminiwa na kuongezewa Bajeti ya toka Wizara ya Fedha kiasi cha Bilion 207 ikiwa ni dhamira ya dhati ya Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan katika kufikia adhma ya Upatikanaji wa Maji safi, salama na yenye kutosheleza.

Kikao hicho kilichofanyika mkoani Dodoma kimehusisha uongozi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), Wakurugenzi Makao Makuu, Mameneja wa Mikoa yote (Regional Managers) na Mameneja wa Wilaya zote (District Managers).

Aidha ameweka bayana Maono, Mipango, Dira, Mikakati na kuweka Malengo kuelekea utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Maji na kuwasihi kuifanya kazi ya uhakika kwa ajili ya watanzania.





Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2