CHIPUKIZI WA BONGO FLEVA WALIA NA MASHABIKI KUTOWAPA NAFASI YA KUWASIKILIZA | Tarimo Blog

Khadija Seif, Michuzi TV

MSANII Chipukizi wa Muziki wa kizazi kipya 'Bongo Flava' Simon Emmanuel maarufu kwa jina la 'Saykiller' amesema bado hali ni ngumu kwa wasanii wachanga katika kupenya kwenye kiwanda cha muziki nchini.

Saykiller ametoa kauli hiyo leo alipokua akizungumza na Michuzi TV, ambapo amesema bado wasanii chipukizi hawapati muda wa kusikika huku akiwatupia lawama mashabiki.

Msanii huyo anaetamba na wimbo wake uitwa 'Poison' amesema wasanii chipukizi inawawia ngumu kupenya kwenye kiwanda cha muziki kutokana na mashabiki na wadau kuwapa nafasi zaidi wasanii wenye majina makubwa.

" Bado kuna kasumba kubwa sana ya kuwapa attention wasanii wenye majina makubwa, sisi ambao bado hatujatoboa inakua ngumu kupewa nafasi, tuna kazi kubwa ya kubadilisha tasnia yetu.

Unakuta chipukizi anapeleka kazi kwenye Redio au TV lakini kama hutojiongeza na kusumbua watu kwa kuhamasisha ipigwe basi unaweza usisikie wimbo wako ukichezwa kabisa," Amesema Saykiller.

Ameeleza kuwa utofauti wake na wasanii wengine upo katika uandishi wake pamoja na utulivu katika kutafuta melody na midundo anapokua anatengeneza ngoma yake.

" Mimi sifanyi muziki kwa kuangalia fulani anafanyaje, ninachoangalia ni kiu ya mashabiki mtaani wanahitaji nini na kwa wakati gani, niwaombe mashabiki wapokee kazi yangu mpya na wanipe sapoti yao," Amesema Saykiller.


 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2