WANIGERIA WAWILI DAR WAFIKISHWA KORTINI KWA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA KILO 10.6 | Tarimo Blog

Na Karama Kenyunko Michuzi TV

RAIA wawili wa Nigeria,  Prince Uche Igwilo( 39) mkazi wa Bunju na Hanifa Ally Chig'wele( 22) mkazi wa Tegeta kwa Ndevu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na shtaka la kusafirisha kilo sita za dawa za kulevya aina ya Heroine.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo leo Juni 9,2021 na Wakili wa Serikali Yusuph Abood mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Joseph Lwambano  imedai, washtakiwa walitenda kosa hilo Mei 22,2021 eneo la Machinjioni Tegeta ndani ya Wilaya ya Kinondoni.

Imedaiwa siku na mahali hapo, washtakiwa walikutwa wakisafirisha kilo 6.10 za dawa za Kulevya aina ya Herione.Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za dawa za kulevya.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 22, mwaka 2021

Wakati huo huo, Oje Ameji Boniface ambaye ni raia wa Nigeria anayeishi Mbezi Makabe anadaiwa kuwa, Mei 24,2021 katika maeneo ya Mbezi beach, Mbezi Makonde na eneo la Mpakani Ubungo  alikutwa akisafirisha gramu 316.4 za dawa za kulevya aina ya Cocaine.

Mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za dawa za kulevya.  Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 22, 2021.



 


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2