FAHAMU MENGI MAKUBWA YA Infinix NOTE 10 PRO | Tarimo Blog


Habari, nitachambua moja ya simu mpya za mkononi yenye kufanya vizuri katika soko la simu kwa sasa. Kampuni ya Infinix Hivi karibuni imezindua rasmi Infinix Note 10 na Note 10 Pro na sifa kuu ya simu hii ni ufanisi wa kiprocess wa Helio G95. kupitia makala hii nitachambua kila kipengele chenye kuunda simu hii.

Kumbuka kuwa simu hizi zipo za aina mbili lakini leo nitaongelea zaidi Infinix NOTE 10pro basi tuanze kwa kuzitaja sifa za simu hii na kisha tuendelee na faida ya kila sifa.

Processor: MediaTek Helio G95
Kamera nyuma: (64MP+8MP+2MP+2MP) AI
Selfie Kamera: (16MP) AI
Memory: 8RAM+128ROM/256ROM
Screen: 6.95FHD+
Resolution: 1080 x 2460
Battery: 5000mAh.

Processor
Kwa upande wa processor, Simu hii ya Infinix Note 10 Pro inakuja na processor ya Helio G95 ambayo ni processor bora sana ambayo hii inajulikana kama Premium 4G Gaming Processor, ambayo ni processor bora sana kwa wapenzi wa game na watumiaji kwa ujumla. Processor hii pia inakuja na uwezo wa RAM ambapo ni mkubwa zaidi hadi GB 10 lakini kwenye simu ya Infinix Note 10 Pro unapata kati ya GB 8.

Kamera
Kwa upande wa kamera simu hii inakuja na kamera nzuri sana ambayo ni bora kulinganisha na simu nyingi. Infinix Note 10 Pro inakuja na kamera ya selfie ya MP 16 ambayo inasaidiwa na flash kupiga picha nzuri zaidi, mbali na hayo kwa nyuma simu hii inakuja na kamera kuu ya Megapixel 64 na nyingine tatu ambapo kwa ujumla unapata kamera nne.

Kamera zote za mbele na nyuma zinakuja na uwezo wa kuchukua video hadi 4K, hii ni moja kati ya sifa ambazo huwezi kuona kwenye simu nyingi za bei hii.

Pia kamera zote za mbele na nyuma zina portrait bokeh mode ambapo unaweza kuziba vitu vya nyuma na kuchukua picha ya mtu au kitu pekee kwa mbele.

Infinix Note 10 Pro pia inakuja na Night Mode kwenye kamera zote za mbele na nyuma, na pia unaweza kupiga picha zenye ubora sana kwa kutumia Night Mode 4K. Mbali na hayo utaweza ku-zoom hadi 10X ambapo utaweza kuona vitu vilivyopo mbalimbali na wewe kwa urahisi.

Display
Kwa upande wa display, Infinix Note 10 Pro inakuja na display ya Inch 6.95 FHD+, diplay hii inafanana kabisa kwa muonekano na toleo la mwaka jana la Infinix Note 8 lakini pia kuna tofauti mkubwa sana. Infinix Note 10 Pro inakuja na kioo chenye uwezo wa 90 Hz refresh rate, pamoja na resolution ya hadi 4k sawa na 1080 x 2460 pixels.

Battery
Kwa upande wa battery, Infinix Note 10 Pro inakuja na battery kubwa ya 5000 mAh Battery, battery ambayo ina uwezo wa kudumu na chaji kwa muda mrefu kulingana na matumizi yako ya kila siku. Ukiwa unacheza game unaweza kucheza kwa muda wa zaidi ya masaa 11 na kubakiwa na battery angalu asilimia 30 kulingana na aina ya game unayo cheza.

Pia simu hii inakuja na teknolojia ya Fast charging 33W ambayo unaweza kuchaji simu hii kwa haraka kwa wale wenye haraka kama mimi. Kwa mujibu wa majaribio yangu, Simu hii ina uwezo wa kujaa chaji kwa hadi asilimia 50 hadi 60 kwa muda wa dakika 30, na kwa muda wa lisaa unaweza kupata chaji kwa 100.

Mbali na hayo kwa kutumia battery ya simu hii unaweza kuchaji simu nyingine kupitia waya wa OTG, pia unaweza kuhamisha data mbalimbali kama utakuwa una waya original wa OTG.

Muundo
Kwa upande wa upande wa muundo, Infinix Note 10 Pro inakuja na rangi tatu ambazo ni Black, Violet, pamoja na Aurora. Mbali ya hayo tukiangalia kwa juu, simu hii haina kitu chochote. Kwa upande wa kulia kuna kitufe cha kuwasha ambacho pia kinafanya kazi kama fingerprint, pia kuna sehemu ya kuongeza sauti na kupunguza, kwa upande wa kushoto kuna sehemu ya kuweka laini za simu pamoja na sehemu ya Memory Card.

Kama ulikuwa hujui, simu hii ya Infinix Note 10 Pro inakuja na uwezo wa kuchukua Memory Card yenye uwezo wa hadi TB 2.

Kwa chini simu hii inakuja na sehemu ya kuchomeka headphone, sehemu ya uwazi wa spika, (spiker grill) sehemu ya Mic pamoja na sehemu ya kuchomeka USB kwa ajili ya kuchaji pamoja na data.

Kitu cha muhimu kufahamu ni kuwa simu hii inakuja na spika mbili juu na chini hivyo simu hii inaweza kutoa sauti kubwa sana, kama wewe ni mpenzi wa game utapenda sana simu hii.Bei na Upatikanaji

Kwa upande wa bei na upatikanaji, Infinix Note 10 Pro inakuja kwa bei nafuu na unaweza kupata sehemu yoyote Tanzania nzima ikiwa na ofa ya GB 78 za Tigo Mwaka Mzima lakini pia unaweza kununua Infinix NOTE 10 kupitia App ya NILIPE. Tafadhali tembelea kurasa za Instagram za Infinix Tanzania kwa taarifa zaidi hakikisha pia unaweza kutembelea https://bit.ly/39gcNcZ au piga nambari ya simu 0744606222.

Tafadhali jaza survey hii https://bit.ly/3gwwK1b kwa kampuni ya Infinix kupata maoni yako kuhusiana na simu hii na Infinix itakuzawadia GB5 za internet.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2