Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na utawala bora Mhe. Haroun Ali Suleiman akizungumzia dhamira ya serikali ya kutaka kuimarisha maslahi ya wafanyakazi kupitia mapitio ya sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idris AbdulWakili Kikwajuni.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akielezea dhamira ya serikali ya awamu ya nane ya kutatua changamoto za wafanyakazi kupitia mfumo na utaratibu wa kukokotoa maslahi ya wafanyazi katika kilichofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idris AbdulWakili Kikwajuni.
Picha ya pamoja.
Washiriki wa Kikao maalum cha kujadili utaratibu wa kukotoa mafao ya watumishi wakifuatilia kwa karibu houtuba ya Mgeni Rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kilichofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idris AbdulWakili Kikwajuni.
PICHA NA OMPR
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kufanya mapitio na marekebisho ya sheria ya mfuko wa Hifadhi ya jamii Zanzibar (ZSSF) kwa lengo la kuzingatia maslahi ya watunishi wake.
Mhe. Hemed, alieleza hayo wakati akaifungu kikao maalum cha kujadili utaratibu wa kukokotoa mafao ya watumishi kupitia mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar kilichofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idris Abdulwakil kikwajuni jijini Zanzibar.
Alisema kuwepo kwa sheria ya mfuko wa hifadhi ya jamii kunalenga kulinda na kuthamini maslahi ya kundi kubwa la wananchi ambao ndio nguvu kazi ya taifa waliokuwepo kazini na wale wanaofikia umri wa kustaafu.
“ Serikali imeandaa mipango madhubuti katika kuhakikisha mafao ya wastaafu yanapatikana ndani ya wakati bila ya kuonewa ama kudhulumiwa mtu yoyote” Alisema Makamu wa Pili
Makamu wa Pili wa Rais alieleza kuwa serikali imekuwa ikifanya marekebisho ya mara kwa mara ya sheria ya mfuko huo inayotokana na sheria namba mbili (2) ya mwaka 1998, ambayo ikafanyiwa tena marekebisho mwaka 2005 na kurekebishwa tena mwaka 2016 inaonesha wazi kuwa serikali imekuwa ikifanya hivyo ili kuhakiha inalinda maslahi na mafao ya wastaafu.
Katika kikao hicho Mhe. Hemed aliwashauri viongozi wanaosimamia mfuko wa Hifadhi wa ZSSF kuangalia na kubadilishana mawazo na viongozi wa mifuko ya hifadhi kutoka Tanazania Bara kwa lengo la kuangalia namna walivyofanikiwa kuzitatua changamoto mbali mbali zilizokuwa zikilalamikiwa na wafanyakazi.
Aidha, Makamu wa Pili wa Rais aliwashauri washiriki wa mkutano huo kutoa mapendekezo yao kwa uwazi kwa tume ya kurekebisha sheria maoni ambayo yataisaidia tume hiyo kupata muelekeo mzuri wa kuwa na sheria bora zaidi itakayoondoa mapungufu yaliyopo sasa.
Nae, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na utawala bora Mhe. Haroun Ali Suleiman alisema tume ya kurekebisha sheria Zanzibar imeamua kufanya mapitio ya sheria hiyo kutokana na malalamiko kutoka kwa wafanyakazi juu ya mfumo uliopo sasa wa kukokotoa maslahi ya wafanyakazi kukumbwa na changamoto.
Waziri Haroun alisema serikali kupitia wizara anayoisimamia itahakikisha maslahi ya wafanyakazi yanaimarika na kuhakikisha haki za wafanyakazi zinapatikana bila ya upenedeleo wowote.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tume ya kurekebisha Sheria Zanzibar Bi Khadija Shamte alieleza kuwa maandalizi ya kikao hicho yanatokana na alioyoyazungumza Mhe. Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Mwinyi katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi kitaifa kwa kutoridhiswa kwa mfumo wa kukokotoa maslahi ya wafanyakazi uliokuwepo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment