Huawei yazindua Bidhaa Mpya Zinazoendeshwa na Mfumo wake wa HarmonyOS 2 | Tarimo Blog

[Shenzhen, China, Juni 6, 2021] Huawei imezindua simu janja (smartphones), saa janja(smartwatches) pamoja na kompyuta bapa(tablet) vinavyotumia mfumo wake mpya wa kiuendeshaji unaoitwa HarmonyOS 2 , utakao wapa wateja wake huduma bora na zinazoweza kujiendesha kutokana na matumizi ya mtu katika nyakati tofauti.

Mbali na mfumo huo, HUAWEI pia imetoa matoleo mapya ya HUAWEI Mate 40, HUAWEI Mate X2, HUAWEI WATCH series 3 na HUAWEI MatePad Pro.

"Kimoja kama vyote, vyote kama kimoja. Tunaishi kwenye ulimwengu ambao vitu vyote vimeunganishwa na vinaweza kujiendesha. Hakuna mtu hata mmoja anaeweza kuukwepa ulimwengu huu." Alisema Richard Yu, Mkurugenzi Mtendaji wa HUAWEI.

Katika hafla hiyo, Huawei pia imezindua HUAWEI FreeBuds 4, vishika sauti(wireless earphones) vya teknolojia ya kisasa vyenye uwezo wa kuzuia kelele za nje(Active Noise Cancellation) huku vikiunganishwa na simu kwa mfumo wa “Bluetooth”. Kampuni hiyo pia imezindua "monitors" mbili zenye ubora wa juu ambazo ni HUAWEI MateView na HUAWEI MateView GT.

HUAWEI ilichukua fursa hio kutangaza kuwa takribani vifaa 100 vya HUAWEI - simu pamoja na kompyuta bapa – vitaboreshwa ili viweze kutumia mfumo huu mpya wa HarmonyOS 2, huku ikiwapa watumiaji wake nafasi ya kufurahia mfumo huu unaoendeshwa kwa utashi na unaoweza kuunganisha vifaa vingi katika hali mbalimbali.

"Kuna vifaa janja(smart devices) vingi katika maisha yetu hivi sasa kuliko hapo awali, lakini ufanisi wake mara nyingi sio mzuri. Ni vigumu kuunganisha mifumo tofauti na kufanya kazi ipasavyo, jambo ambalo huupelekea watumiaji kutoridhika." Alisema

"HarmonyOS imetengenezwa kushughulikia tatizo hilo. Mfumo huu hutoa lugha ya kawaida kwa vifaa mbalimbali ili viweze kuunganishwa pamoja na kushirikiana, huku ikiwapa watumiaji ubora, ufarisi na usalama wa hali ya juu." Alisema Yu

HarmonyOS 2 hutumia teknolojia kukidhi mahitaji tofauti ya vifaa mbalimbali hivyo kuongeza urahisi katika matumizi. Mfumo huu pia hujumuisha vifaa vilivyokua vinajitegemea kwenye mfumo wake na kuvifanya kuwa kifaa kimoja chenye uwezo mkubwa ambacho huunganisha rasilimali zote na kuzielekeza kutokana na matumizi halisi ya mtu.

"Kwa watengenezaji wa programu, HarmonyOS 2 hutoa jukwaa la kutengeneza programu ambazo zinaweza kuingiliana na mifumo mingine na hivyo kufanya ukuaji wa program kuwa rahisi kuliko hapo awali." Alimalizia




Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2