KAMPUNI 15 KUTOKA MISRI ZAPIGA KAMBI DAR KUONESHA BIDHAA ZAO | Tarimo Blog





Baadhi ya wafanyabishara kutoka nchini Misri wakiuza bidhaa zao wakati wa maonesho hayo.
Balozi wa Misri nchini Tanzania  Mohamed Gaber Abulwafa akizungumza wakati wa maonesho hayo ua bidhaa za kutoka kwa Kampuni za Misri ambazo zimekuja nchini Tanzania kuonesha bidhaa zao.
Mwakilishi wa Waziri wa Viwanda na Biashara Profesa Kitila Mkumbuko, Edwin Rutageruka akifafanua jambo wakati akizungumza kwenye maonesho hayo ya bidhaa za kampuni kutoka Misri


Na Emilion Sanya, DSJ

KAMPUNI 15 kutoka nchini Misri zimekuja nchini Tanzania kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu wa wafanyabiashara wa Watanzania.

Akizungumza leo Mei 17 ,2021 wakati wa maonesho madogo ya bidhaa za kampuni hizo, Muwakilishi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Edwin Rutageruka amesema lengo na dhumuni ya kampuni hizo kuja nchini ,ni kutaka kuona mazingira ya kibiashara nchini ili kupanua wigo wa soko la bidhaa baina ya nchi hizo mbili.

Amesema wafanyabiashara hao kupitia kampuni zao wamekuja na bidhaa mbalimbali ikiwemo  dawa binadamu, mbolea pamoja na kemikali mbalimbali.

Aidha amesema licha ya kampuni hizo  kutaka kujua watawezaje kuja kufanya biashara yao hapa Tanzania ni kwamba Watanzania  wanaweza  kunufaika sana ,hivyo ni wakati wa kuchangamkia fursa kwa kuzalisha kahawa ,na kupeleka  Misri.

Amezitaka kampuni zinazojishughulisha na utengenezaji vifungashio nchini kuchukua au kupata ujuzi wa kutengeneza vifungashio vilivyo bora na imara kwa maana wenzetu egypt vifungashio vyao viko vizuri na kwa ubora zaidi.

Ameziomba  kampuni hizo kutoka Misri kuja kuwekeza nchini kwenye maeneo ya viwanda  vya kutengeneza nguo." Kama tunavojua upatikanaji wa ngozi hapa Tanzania ni wakutosha hivyo si mbaya kama wakifungua kiwanda cha uzalishaji mikoba au mabegi,viatu vya ngozi ,na hivyo kunufaika sote."

Pia amewataka vijana kuchangamkia fursa ya kuwa hata mabalozi wa kusambaza bidhaa hizo.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2