TPB YAINGIA MAKUBALIANO NA ALLIANCE LIFE ASSURANCE KWA LENGO LA KUTOA BIMA YA MAISHA KWA WATEJA WAKE | Tarimo Blog

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta TPB Saba saba Moshingi (kulia) akibadilishana hati ya makubaliano na Mkurungezi kutoka Kampuni ya Alliance life Assurance, Byford Mutimusakwa,(kushoto) baada ya kuzindua Bima ya Maisha kwa wateja wa benki hio. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.


Na Mwandishi Wetu

BENKI ya TPB imeingia  makubaliano na Kampuni ya Bima ya  Alliance life Assurance kwa ajili ya kutoa bima ya maisha kwa wateja wenye akaunti binafsi katika benki hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dar es salaam katika  hafla hiyo Mkurungezi wa Benki ya TPB, Sabasaba Moshingi amesema  bima hiyo itatolewa kwa wateja wenye akaunti binafsi benki hiyo  dhidi ya tukio la kifo cha mteja, mwenza na ulemavu wa kudumu wa mteja unaotokana na ajali.

Amesema benki hiyo imekuwa ikitambua umuhimu wa  bima katika maisha ya binadamu hivyo imeona ni vema kuungana na Kampuni ya Alliance life Insurance kuwawezesha wananchi kupata huduma hiyo.

"Benki ya TPB imekuwa ikitambua umuhimu wa bima katika maisha ya binadamu na kwa sasa nchi yetu imekuwa ikikabiliwa na ufinyu wa watu katika kujiandikisha katika bima mbalimbali"alisema

Moshingi amesema huduma hizo azitakuwa na gharama ya juu kwa  mteja huku alisisitiza kuwa mafao hayo ni kwa ajili wamiliki na mmiliki wa akaunti tu na mteja ni lazima awe na akaunti ya akiba na iwe hai.

Awali Mkuu wa kitengo cha Bima TPB , Francis Kaaya amesema katika bima hiyo kutakuwa kukitolewa mafao mawili ambayo ni pamoja na fao la kifo na fao la ulemavu wa kudumu.

"Fao la kifo ni fao kwa wateja wenye akaunti za akiba dhidi ya tukio la kifo cha mmiliki wa akaunti, mwenza na watoto wasiozidi wa nne"amesema Kaaya na kuongeza kuwa TPB itatoa kifuta machozi kwa mteja au familia Kama rambirambi ili kutatua baadhi ya gharama zinazohusu mazishi.

Katika fao la ulemavu wa kudumu Kaaya alisema hili fao ambalo litapatikana kwa mteja au wateja ambaye ni mmiliki wa akaunti anayekabiliwa na ulemavu wa kudumu uliotokana na ajali.

Kwa upande wake Mkurungezi kutoka Kampuni ya Alliance life Assurance, Byford Mutimusakwa alisema bima ni muhimu katika maisha kila mtu hivyo aliipogeza benki ya TPB kwa kuhakikisha wateja wake wanapata huduma hiyo.

"Kwa sasa wateja wa benki ya TPB wataweza kupata bima hii ya nishike mkono pasipo na usumbufu wote"amesema.

Aidha aliwataka wananchi kiwa na tabia ya kutumia bima ili kuepuka majanga mbalimbali katika maeneo wanayoishi na wanayofanya kazi.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2