Kuelekea siku ya Mazingira Duniani jamii yaaswa kutunza Mazingira | Tarimo Blog

Jane Edward Michuzi TV, Arusha


Kuelekea kilele Cha maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani bado kumekuwepo na changamoto ya kuharibika kwa mifumo ya ikolojia ambapo kumesababisha madhara makubwa ikiwemo ukataji miti holela ,utiririshaji maji machafu kwenye mito,maziwa, sambamba na utoaji gesi joto kutoka kwenye mitambo mbalimbali viwandani na vyombo vya usafiri .

Hayo yameelezwa na meneja wa baraza la Taifa la usimamizi wa Mazingira Mkoani Arusha (Nemc) Lewis nzali Wakati wa kikao na waandishi wa habari kilichofanyika ofisi za Baraza hilo huku kauli mbiu ikiwa ni Tutumie Nishati mbadala kuongoa mifumo ya Ikolojia.

Katika kufikia dira nadhima ya Baraza hilo kufanya tahmini ya athari kwa mazingira kukuza uelewa kwa wananchi kuhusu mazingira kuratibu shughuli za usimamizi wa mazingira na kufanya tafiti za mazingira ili kuongoa mifumo ya ikolojia.

Lewis ameongeza  kuwa uharibifu wa mifumo ya ikolojia unahatarisha Sana biashara ambapo mifumo hii ikiharibika inaharibu uchumi ambapo kwa sasa dunia imekuwa ikikabiliwa na majanga yanayosababishwa na uharibifu wa mifumo ya Ikolojia.

Aidha amesema kuwa mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanasababisha mvua zisizo na mpangilio,ongezeko la joto , kuharibika kwa miundombinu  sambamba na kuongezeka kwa kina Cha maji kwenye bahari na maziwa .

Amebainisha kuwa jukumu la utunzaji wa Mazingira ni la kila mtu, na hakuna dunia nyingine zaidi ya hii, hivyo ni wajibu jamii ikatunza Mazingira yetu kwa ustawi wa Afya na maendeleo endelevu. 




Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2