WILAYA ya Lushoto imeingia dosari baada ya Mwenge wa Uhuru kutozindua mambweni ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Magamba kufuatia wakimbiza mwenge kutoridhishwa na utandikaji wa mfumo wa maji safi na maji taka.
Akizungumza baada ya kukagua,Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa 2021,Josephine Mwambashi amesema hawezi kuzindua mabweni hayo kwa sababu yatakapoanza kutumiwa kuna hatari ya wanafunzi kukumbwa na magonjwa ya milipuko.
"Hatutauzindua mradi huu kwa sababu mfumo wa maji safi na maji taka ni mbovu...tunachoagiza ni wahandisi waje wafanyie marekebisho halafu Mkuu wa Wilaya utatafuta njia nyingine ya kuuzindua" alisema Mwambashi.
" Nawaagiza Taasisi ya Kupambana na kuzuia Rushwa(Takukuru) mkachunguze mara moja wasimamizi wa mradi huo wa mabweni pia Naagiza Mkuu wa wilaya pia ahakikishe anachua hatua kwa wahusika sababu wameudanganya Mwenge wa Uhuru." aliagiza Mwambashi.
Mwenge wa Uhuru kazi yake ni kumulika na kuleta matumaini pale ambapo hakuna matumaini hivyo wahusika wachukuliwe hatua sababu wamefanya udanganyifu na wameudanganya mwenge wa Uhuru .
"Kwa muda mfupi mikoa michache tuliyotembelea tumeona hakuna uwazi,hakuna mipango mizuri na hukuna uwajibikaji katika kuzisimamia fedha za umma kuleta maendeleo ya taifa"Alisema Kiongozi huyo.
Mkuu wa shule hiyo,Peter Nyero alisema mabweni hayo yatakapozinduliwa yatatumiwa na jumla ya wanafunzi 160 ambao walikuwa hawana mahala pa kulala.
Hata hivyo Mabweni hayo ni kwa ajili ya kulala wanafunzi wa kidato cha tano na sita wa tahasusi ya sayansi wa shule hiyo yamejengwa kwa gharama ya sh 19,529,148 zikiwamo sh 150,000,000 zilizotolewa na Serikali kuu.
Ukiwa Wilayani Lushoto, Mwenge wa Uhuru ulizindua kuweka mawe ya msingi na kukagua jumla ya miradi 12 yenye thamani ya sh 2.1.bilioni ambayo fedha zake zimetolewa na Serikali kuu, Haashauri ya Wilaya ya Lushoto, mfuko wa jimbo na nguvu za wananchi.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment