NAMTUMBO YAKOPESHA ZAIDI YA MILIONI 172 KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU. | Tarimo Blog

 

NA YEREMIAS  NGERANGERA…NAMTUMBO.

Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Mkoani  Ruvuma  kwa kipindi cha miaka sita 2015/2016  hadi  2020/2021 imekopesha  vikundi 229 wenye  wanachama  zaidi ya 800 jumla ya shilingi  milioni 172,500,000.

Afisa  maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo bwana  Peres  Kamugisha aliyasema hayo kwenye semina elekezi  ya ujasilimali na maendeleo ya biashara  kwa vikundi vilivyopatiwa mkopo katika halmashauri hiyo.

Bwana Kamugisha alisema  halmashauri imelazimika kutoa semina elekezi  kwa vikundi vilivyopatiwa mkopo ili kuwa na uelewa  kuhusu namna  ya kufanya  shughuli za  ujasiliamali na kuwa na maendeleo  ya kweli katika biashara zao  na waweze kulipa mikopo  wanayopewa kadiri ya sheria ya mikopo  za mwaka 2021.

Alisema  zipo changamoto kubwa ya  baadhi ya vikundi  kutokuwa na uaminifu  na kupelekea  kutorejesha mikopo kwa wakati  licha ya kuwapatia semina elekeza ya ujasiliamali pamoja na namna  ya kuendesha biashara  zao mara kwa mara.

Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Sophia Mfaume Kizigo alialikwa katika semina hiyo na kuwataka wanufaika ya mikopo ya vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kuzitumia fedha hizo  katika malengo yaliyokusudiwa .

Kizigo alidai wapo wanaopata mkopo na hawataki kurudisha hali inayokwamisha vikundi vingine vyenye uhitaji wa kupata mikopo hiyo kukosa kupatiwa mikopo kutokana na baadhi ya vikundi kutokuwa waaminifu wa kurudisha mikopo.

Wapo  walemavu wanaowezeshwa kupata mikopo ili wajiinue kimapato lakini wapo wengine wanatumia kigezo hicho cha ulemavu kama kinga ya kutorudisha  mikopo na wanaposhindwa kurudisha mikopo wanajizuia kupata mkopo tena .

Aliwataka  walemavu  kutojiona kuwa wao ni tofauti na makundi mengine bali kuwa wao ni sawa na makundi mengine na wanatakiwa kupata mikopo na kuirudisha ili waendelee kuaminiwa na serikali na  kukopeshwa mara kwa mara.

Asha  kamtende ni mnufaika wa mkopo kutoka katika kikundi cha wajasiliamali nguvu moja pamoja na kuishukuru serikali kuwajali wajasiliamali wadogo kwa kuwapatia mikopo alisema  kikundi chao kimewezeshwa kupata 1,500,000 na wataitumia fedha hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa na kasha kurudisha mkopo huo kwa wakati  ili serikali iwaamini na kisha kuendelea kukopeshwa mara kwa mara.

Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo  kwa mwaka fedha  2020/2021 hadi mei  halmashauri imetoa kiasi cha shilingi   80,000,000 kupitia mapato yake  ya ndani kwa vikundi 25 vya wanawake ,vijana na watu wenye ulemavu  vyenye jumla  ya wanachama 60 ambapo kwa miaka sita jumla ya shilingi milioni 172,500,000 zimekopeshwa kwa vikundi vya vijana 94, vyenye wanachama310 vimepatiwa mkopo wa shilingi 168,800,000,vikundi vya watu wenye ulemavu vikundi 26 vyenye wanachama zaidi ya 70 jumla ya shilingi 47,000,000  zilikopeshwa  na saccos ya vijana moja jumla ya shilingi 5,350,000.

Picha ya baadhi ya vikundi wakiwa katika semina elekezi ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo pamoja na picha ya pamoja iliyopigwa wakiwa na mkuu wa wilaya ya Namtumbo Sopihia mfaume Kizigo nje ya ukumbi wa Halmashauri

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2