MWENGE WA UHURU WAWASILI TANGA | Tarimo Blog

 





Raisa Said,Tanga

WAZAZI na walezi Nchini wametakiwa kuhakikisha wanatumia vyakula lishe ili  kujenga mwili na akili kwa Watoto wao.

Wito huo umetolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Josephine Mwambashi alipokuwa anatoa ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru  kwa Mwaka huu 2021 baada ya kuwasili katika wilaya ya  Muheza ,Pangani na Mkinga Mkoani Tanga.

Mwambashi alisema  Mbio za Mwenge zinaendelea kusisitiza kuhusu  matumizi sahihi  ya lishe bora  ambapo alieleza lishe bora kwa watoto wetu ni jukumu la kila mzazi na ni haki ya kila mtoto kuipata.

Ili watoto wakue kimwili na kiakili ni lazima wapate lishe bora ambayo itawasaidia kuwa vijana shupavu na nguvu kazi ya Taifa .

Pia amesisitiza Wajawazito kufika katika vituo vya afya ili waweze kuwapatiwa elimu inayotolewa kuhusu uandaji wa lishe bora na Sahihi kwa mtoto .

 "Lishe bora si lazima ulaji wa chakula kingi bali  lishe bora ni ulaji wa vyakula mchanganyiko vya lishe ikiwemo   matunda,mbogamboga,asali"Alisisitiza Kiongozi wa Mwenge Kitaifa  Josephine Mwambashi.

Hata hivyo Kiongozi huyo alieleza Mbio za Mwenge pia zinaendelea kusisitiza mapambano dhidi ya malaria chini ya kauli mbiu isemayo ziro malaria inaanza na Mimi na chukua hatua kuitokomeza.

Alisema ugonjwa wa malaria bado  upo na unatesa sana watoto na wajawazito hivyo tujitahidi kupambana nayo kwa kulala kwenye vyandarua vyenye dawa kufukia madimbwi   ili kuuwa vimelea vya mazalia ya mbu na kufanya usafi katika mazingira yanayotuzunguka.

Ili kuendelee kuwa na nguvu kazi na kulea watoto wenye afya nzuri ni lazima tuendelee kupambana na ugonjwa huo.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2