Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amewataka Madiwani wa Jijini la Dar es salaam kuepuka Migongano na Mivutano isiyokuwa na faida yoyote kwa Wananchi na badala yake wajikite Katika kujenga hoja na Mipango ya kutatua kero kwa maslahi mapana ya Wananchi.
RC Makalla amesema kumekuwa na katabia ka ajabu pale Serikali inapotoa fedha kwaajili ya utekelezaji wa miradi fulani, Madiwani wanajikuta wanaanza kulumbana kwa Mambo yasiyokuwa na msingi Jambo linalochelewesha kuanza kwa miradi ya maendeleo na kuleta usumbufu kwa Wananchi.
Akizungumza wakati wa kikao Cha pamoja kati yake na Madiwani pamoja na Maafisa Watendaji kata, RC Makalla amewataka Viongozi hao kusimamia kikamilifu suala la Usafi Katika maeneo yao na kuwa mstari wa mbele kwenye usimamizi wa miradi ya maendeleo.
Aidha RC Makalla ameonyesha kufurahishwa na mafanikio makubwa yanayoendelea kupatikana katika Operesheni tokomeza Majambazi na Vibaka Dar es salaam ambapo amewahakikishia wananchi kuwa Serikali imejidhatiti kuwalinda na Mali zao.
Hata hivyo RC Makalla amelitaka Jiji la Ilala kuhakikisha linawapanga Vizuri Wamachinga Katika maeneo yao ili Waweze kufanya Biashara zao kwa Hali ya Usalama na kwa mujibu wa Sheria.
Pamoja na hayo, RC Makalla amelitaka Jiji la Ilala kuhakikisha Mradi wa Machinjio ya kisasa Vingunguti unaanza kufanya kazi ifikapo July mosi ili lengo la kuanzishwa kwa Machinjio hayo litimie.
Kwa upande wao Madiwani na Maafisa watendaji kata wamemuhakikishia RC Makalla kuwa maelekezo na Maagizo aliyoyatoa wameyapokea kwa mikono miwili na watayafanyia kazi kuanzia leo.
Aidha wamempongeza kwa uamuzi wake wa kuanza ziara ya Kata kwa Kata na wamemuahidi kumpatia ushirikiano kwakuwa wanaamini kupitia ziara hiyo watu wengi watatatuliwa kero zao.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment