Akitoa tamko la tahadhari dhidi ya Corona RC Makalla amesema kutokana na mwingiliano wa watu kutoka nchi jirani na nchi za nje na Mikoa mingine wameona ni vyema kutoa tahadhari kwa Wananchi.
Miongoni mwa tahadhari ambazo RC Makalla amewataka Wananchi kuzichukuwa ni pamoja na :-
1.Kuvaa kwa Usahihi Barakoa kila wawapo sehemu za mikusanyiko, vyombo vya usafiri, Masoko, sherehe, maofisini na vituo vya Afya.
2. Kunawa mikono kwa maji tiririka kwa sabuni mara kwa mara.
3.Wananchi kuwahi mapema vituo vya Afya wanapobaini dalili za Corona ikiwemo homa kali, mafua makali, kikohozi, uchovu na nyinginezo.
4. Kufanya mazoezi ili kuimarisha kinga ya mwili.
5. Kula mlo kamili.
6. Uangalizi mzuri kwa watu walio kwenye hatari ya kupata madhara wakiwemo Wazee na wenye magonjwa sugu.
Aidha RC Makalla amewaelekeza Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Taasisi za Umma na za kiraia na Vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanasimamia ipasavyo maelekezo hayo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment