RUWASA HAKIKISHENI VIJIJI VYOTE VINAPATA MAJI | Tarimo Blog

 Raisa Said,Muheza


KIONGOZI wa mbio za Mwenye kitaifa Luteni Josephine Mwambashi  amesema amefurahishwa na uwajibikaji wa Wakala  usambazaji maji vijijini RUWASA Mkoa wa Tanga  kwa namna walivyotekeleza miradi yao kwaviwango vya juu huku akiwataka wahakikishe vijiji vyote vinapata huduma hiyo muhimu.

Josephine ameyasema hayo jana wakati wa mbio za Mwenye ambao ulifanyika uwekaji wa mawe ya msingi pamoja uzinduzi katika wilaya za Pangani  na Muheza,
Alisema RUWASA Mkoa wa Tanga imejitahidi kutekeleza maelekezo ya Serikali yakuhakikisha Wananchi wanapata huduma ya maji kwakiwan

Akiwa  wilayani  Muheza Aliitaka  RUWASA  kuhakikisha inamalizia miradi mbalimbali iliyoanza na ile iliyopo kwenye bajeti ijayo ," Nimefurahishwa hasa huu mradi mkubwa wa Umba, mradi huu unakwenda kumtua mama ndoo kichwani , endeleeni na kazi nzuri lakini mhakikishe bajeti inayokuja vijiji vyote vinaunganishiwa na huduma ya maji" Alisema Josephine


PANGANI

Huko wilayani Pangani Mwenge uliweka jiwe la msingi katika mradi mkubwa wa maji kwenye kijiji cha Mikocheni kata ya Mkwaka ambapo  Waziri wa Maji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Pangani alimuomba kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa 2021 Josephine Mwambashi asisite kukagua miradi ya maji nchi nzima kwa kuwa ripoti yake itasaidia kuchukua hatua mbalimbali ili zitakazorahisisha  kukamilisha miradi ya maji nchini.

Waziri Aweso alisema Rais Samia Suluhu Hassan  amempatia  dhamana ya kuhakikisha watanzania wanaondokana na tatizo la  ukosefu wa maji safi na salama nchini

"Ndugu zangu watanzania nimepewa dhamana ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama hii dhamana ni kubwa sana hivyo nikuombe kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa usisite katika kila wilaya na mikoa kukagua miradi ya maji inayotekelezwa nchini, "alisisitiza Waziri Aweso.

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kigaigai baada ya Mwenge huo kukimbizwa katika wilaya nane  za mkoa wa Tanga .
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2