Kamishna wa Idara ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. John Mboya akifundisha wahariri (hawapo pichani) kuhusu dhana ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi walioshiriki semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari, jijini Arusha.
Kamishna wa Idara ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. John Mboya akifundisha wahariri kuhusu dhana ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi walioshiriki semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari, jijini Arusha.
Afisa kutoka Idara ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Edwin Kachenje akifutalitia kwa makini wasilisho kwenye kompyuta mkapato wakati wa semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu masuala ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, jijini Arusha.
hariri wa Gazeti la Jamvi la Habari Dkt. Bravious Kahyoza akisoma kanuni za Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wakati wa semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu masuala ya Ubia, jijini Arusha.
Kamishna Msaidizi wa Idara ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Bashiru Taratibu akifafanua jambo wakati wa semina ya wahariri wa vyombo vya Habari kuhusu masuala ya ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, jijini Arusha.
Mhariri wa Star Tv Bw. Dotto Shashi (kulia) na mhariri wa redio Free Afrika Bw. Jilala Duttu wakifuatilia mada iliyowasilishwa wakati wa semina Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu masuala ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, jijini Arusha.
Kamishna wa Idara ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. John Mboya, akimkabidhi cheti cha ushiriki Mwenyekiti wa mkutano wa wahariri Bw. Ben Mwang’onda, baada ya kumalizika kwa semina ya siku mbili ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi iliyofanyika jijini Arusha.
Kamishna wa Idara ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. John Mboya, akimkabidhi cheti cha ushiriki mhariri wa Clouds Media Bi. Joyce Shebe baada ya kumalizika kwa semina ya siku mbili ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi iliyofanyika jijini Arusha.
(Picha na Wizara ya Fedha na Mipango – Arusha)
************************
Na. Josephine Majura, WFM, Arusha
WAHARIRI wa vyombo vya habari wameahidi kuendelea kushirikiana na serikali kutangaza miradi mbalimbali inayotekelezwa nchini ili wananchi wafahamu kazi kubwa inayofanywa kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
Ahadi hiyo wameitoa jijini Arusha wakati wa kufunga semina ya wahariri hao iliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Kitengo cha Mawasiliano Serikalini lengo likiwa kuwajengea uwezo wahariri kuhusu dhana ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP).
Mhariri wa Gazeti la Tanzanite Bi. Selina Mathew, Clouds Media Joyce Shebe, Habarileo Bakari Kingoba, wameipongeza Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuandaa mafunzo hayo kwa wahariri kwani yamewajengea uwezo mkubwa kuelewa dhana ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ambayo bado ni changamoto kwa baadhi ya waandishi katika kuiripoti.
“Wataalamu wametupa shule ya kutosha mambo mengi tulikuwa hatuyafahamu lakini kupitia semina hii ya siku mbili tumejifunza mengi kwa kweli tunaipongeza Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuandaa mada ambazo zimekuwa na tija kwetu na zimetoa mwelekeo wa nini kinafanyika kwenye dhana ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi,” alisema Bi. Selina Mathew.
Waliahidi kwenda kuandika makala za kutosha ili kuelimisha jamii kuhusu dhana ya PPP na namna itakavyoleta matokeo chanya kwa nchi kupitia uwekezaji unaofanywa na Sekta Binafsi katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.
Aidha Wahariri hao walishauri serikali isichoke kutoa elimu na kutangaza miradi inayotekelezwa na serikali na kuongeza kuwa wao kama chombo cha kutoa taarifa kwa umma wataendelea kutoa taarifa mbalimbali kuhusu mafanikio ya serikali ili dhana potofu ya kuwa serikali haitekelezi miradi kwa wakati iweze kufutika.
Kwa upande wake, Bi. Janeth Mushi aliwapongeza wataalamu kutoka Idara ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kwa mada mbalimbali walizofundisha ikiwemo Dhana ya PPP, Sheria na Kanuni zake.
“Sisi ni chombo cha kutoa taarifa kwa umma ni wakati sasa kwa taasisi na wizara nyingne kuiga mfano huu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wa kutujengea uwezo ili tuwe na uelewa mpana wa shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali ili tuweze kuzitangaza na wananchi wajue kazi nzuri na kubwa inayofanywa na serikali”, alisisitiza Bi. Mushi.
Naye Mhariri wa Gazeti la Majira, Bw. Ruben Kagaruki alitoa ushauri kwa Wizara ya Fedha na Mipango iandae mafunzo kwa ajili ya waandishi wa habari kwa kuwa wao ndio wanaenda kuchukua taarifa hivyo ni vizuri nao pia wakapatiwa mafunzo ya masuala ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ili wawe na uelewa mpana katika utekelezaji wa majukumu yao.
Kwa upande wake, Mhariri wa Gazeti la Raia Mwema, Bw. John Daniel, aliishauri serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kusimamia kwa hali na mali utekelezaji wa Sheria na Kanuni za PPP, bila kuruhusu mianya ya rushwa na kupewa watu ambao hawana uwezo wa kutekeleza miradi hiyo na kusababisha ucheleweshwaji na miradi kutokamilika kwa wakati.
Bw. Daniel aliongeza kuwa ni vyema Wizara ya Fedha na Mipango ikaongeza muda wakati mwingine wakiandaa semina ili kutoa nafasi kwao kujifunza mambo mengi kwa weledi zaidi kwa kuwa elimu waliyoipata ni sehemu tu katika dhana nzima ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi.
Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kimekuwa na utaratibu wa kufanya semina na wahariri wa vyombo vya habari nchini lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kutoa taarifa za wizara hiyo kwa usahihi.
Hadi sasa wizara imeshafanya semina kwa wahariri wakitokea kwenye vyombo vya habari zaidi ya 40 katika nyanja mbalimbali kuhusu majukumu yanayotekelezwa na wizara ikiwemo masuala ya Huduma Ndogo za Fedha, Mfumo wa Kielektroniki wa Malipo ya Serikali (GePG) na semina hii ya masuala ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi.
Kabla ya kufunga semina hiyo, Kamishna wa Idara ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi Dkt. John Mboya, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, aliwakabidhi Wahariri vyeti vya kushiriki semina hiyo kwa ufanisi mkubwa.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment