TBS YAKUSANYA SHILINGI BIL.1.9 KUTOKANA NA UKAGUZI WA MAGARI YATOKAYO NJE YA NCHI | Tarimo Blog

 

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 

Katika kipindi cha miezi miwili Shirika la Viwango Tanzania (TBS),limefanikiwa kukusanya shilingi Bilioni 1.9 kutokana na ukaguzi wa magari yanayotoka nje.

Ameyasema hayo leo Meneja wa Ukaguzi wa Bidhaa zinazotoka nje ya nchi (TBS), Mhandisi Saidi Mkwawa katika ofisi za Shirika hilo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Mhandisi Mkwawa amesema kuna umuhimu wa waagizaji wa magari kutumia makampuni kuagiza magari ili kuweza kuepuka kupata hasara kama gari litafika halijakidhi viwango.

Aidha amesema kuwa hapo awali ukaguzi wa magari ulikuwa unafanyika nje ya nchi, Serikali ilikuwa inapata asilimia 30% ya mapato ya ukaguzi ambayo ni sawasawa na Milioni 576.6.

"Hadi sasa ndani ya miezi miwili tumeokoa kiasi cha Bilioni 1.3 ambacho kama magari haya yangekaguliwa nje ya nchi basi fedha hizo zingekuwa katika nchi ambazo zinafanya ukaguzi". Amesema Mhandisi Mkwawa.
Meneja wa Ukaguzi wa Bidhaa zinazotoka nje ya nchi TBS, Mhandisi Saidi Mkwawa akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2