WATANZANIA wameshauriwa kutotumia watu binafsi katika uagizaji wa magari nje ya nchi bali watumie kampuni za uagizaji magari zinazotambulika ili kujiwekea salama linapotekea suala la kuletewa bidhaa zisizokidhi vigezo.
Akizungumza leo wakati akifungua mafunzo kwa Wahariri wa Vyombo vya habari yaliyofanyika Makao Makuu ya shirika hilo mkoani Dar es Salaam,Mkurugenzi mkuu wa TBS, Dkt Athuman Ngenya amesema baadhi ya watu wamekuwa wakitafuta magari katika mitandao na kuwatumia watu binafsi wanaouza magari nje ya nchi na kuishia kuletewa magari yasiyokidhi vigezo ambavyo vimewekwa kwa kampuni za ndani za uagizaji wa magari nje ya nchi na ni rahisi kuwakamata pindi wakikiuka vigezo hivyo.
Amesema kuwa, tangu awali wamekuwa wakitoa semina nyingi kwa kampuni zinazoagiza magari nje ya nchi zikiwemo Be Forward na SBT ambao asilimia 90 ya magari huingia nchini kupitia kwao.
Amesema semina hizo zimekuwa zikielekeza juu ya kanuni na vigezo vya kuzingatia katika mchakato mzima wa uagizaji wa magari na wamekuwa wakifuatilia mrejesho kutoka kwa wanunuzi na kuyafanyia kazi malalamiko yao.
Kuhusiana na utaratibu wa baadhi ya kampuni kuwa na utaratibu wa kuchukua pesa za wananchi na kuwaletea magari mabovu, Ameeleza wamekuwa wakihakikisha magari yanayoletwa yanakidhi ubora.
"Tumekuwa tukifuatilia kupitia kila 'document' za magari yanayoagizwa na kampuni mbalimbali na tukiona magari yanayoagizwa na kampuni X yanalalamikiwa sana na wananchi, kampuni hiyo inawekewa X na tunaiambia Serikali kwamba kampuni hiyo haitakiwi na hili wanalifahamu kwa kuwa wakileta magari mabovu wanaua kampuni zao" Amesema.
Kuhusiana na changamoto ya ubora wa magari yanayoagizwa, amesema asilimia 80 ya changamoto ni tairi ambazo hugharamiwa na mmliki ukilinganisha na changamoto za engine na muonekano wa gari ambazo hutokea mara chache.
Kwa upande wake Meneja wa Ukaguzi wa bidhaa zinazotoka nje ya nchi Mhandisi Said Mkwawa akizungumzia kuhusu ukaguzi wa magari yatokayo nje ya nchi amesema ukaguzi huo pia umefanikisha kukusanya kiasi cha bilioni 1.5 ambazo hapo awali wangepata asilimia 30 pekee
“Katika magari 4779 tulioyafanyia ukaguzi kuanzia mwezi aprili 15 mpaka June 08, asilimia 85 ya changamoto kubwa imejitokeza kwenye ubovu wa kashata,taa, na magurudumu kuisha muda wake”. Amesema Mhandisi Mkwawa.
Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athumani Ngenya akifungua mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari kwa lengo la kuwajengea uwezo na uelewa kuhusu majukumu mbalimbali ya TBS ,Mafunzo hayo yamefanyika leo leo Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Masoko Bi.Gladness Kaseka akiwasilisha mada katika mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari kuhusu majukumu ya TBS yaliyofanyika leo Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Dar es Salaam. Meneja wa Ukaguzi wa Bidhaa zinazotoka nje ya nchi, Mhandisi Said Mkwawa akitoa ufafanuzi katika mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari kuhusu ni namna gani inafanya ukaguzi wa bidhaa na kubaini zinazo kidhi na zisizo kidhi viwango,Mafunzo hayo yamefanyika leo Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Dar es Salaam.
Afisa Udhibiti Ubora wa TBS, Bw.Diocles Ntamulyango akiwasilisha mada iliyohusu ukaguzi wa Magari yaliyotumika yaliowasili nchini, katika mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari , yaliyofanyika leo Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Dar es Salaam .
Mkuu wa Maabara ya Kemia Bw.Charles Batakanwa akiwasilisha mada yake iliyohusu uwekaji vinasaba katika mafuta wakati wa mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari yaliyofanyika leo Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Upimaji na Ugezi wa TBS, Mhandisi Johannes Maganga akizungumza katika hafla ya mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari juu ya majukumu ya TBS yaliyofanyika leo Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Dar es Salaam.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment