WAZIRI MKUU KUWA MGENI RASMI SIKU YA KUADHIMISHA MAPAMBANO YA DAWA ZA KULEVYA ,KITAIFA KUFANYIKA JIJINI DODOMA | Tarimo Blog


Na Said Mwishehe, Michuzi TV.

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imesema Tanzania huungana na mataifa mengine kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya ambapo mwaka kwa mwaka huu kitaifa maadhimisho hayo yatafanyika Jijini Dodoma Juni 6 mwaka huu wa 2021.

Mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa huku lengo kuu la maadhimisho hayo ni kuongeza uelewa wa jamii na kuhamasisha umma kushiriki katika mapambano    ya matumizi na biashara ya dawa za kulevya.

Kamishina Jenerali wa Mamkala ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kelvya  Gerald Kusaya amewaambia waandishi wa habari leo Juni 17,2021 mkoani Dar es Salaam kuwa kitaifa maadhimisho hayo yatafanyika Viwanja vya Nyerere Square na mgeni atakuwa Waziri Mkuu.

Ameongeza kauli mbiu ya mwaka huu kwenye maadhimisho hayo inasema hivi "Tuelimishane juu ya tatizo la dawa za kulevya , kuokoa maisha." na kwamba kauli mbiu hiyo inaelekeza kuwa jamii inatakiwa kujua ukweli kuhusu madhara yanayotokana na matumizi ya dawa za kulevya.

Ameongeza lengo ni kuhakikisha jamii haijiingizi katika matumizi ya dawa hizo ."Hatua hiyo itasaidia kuokoa maisha ya watu wengi ambao wangeangamizwa na dawa za kulevya."Aidha maadhimisho haya yataanza Juni 24 ,2021 na yatatanguliwa na maonesho ya shughuli mbalimbali za udhibiti wa dawa za kulevya zinazofanywa na taasisi za serikali, asasi za kiraia na watu binafsi,"amesema Kusaya.

Amewaomba wananchi na wakazi wa Dodoma kushiriki kwa wingi katika maadhimisho hayo na Mamlaka imewakumbusha Watanzania kuendelea kushiriki katika mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya kwani mapambano hayo ni ya wote.

Kamishina Jenerali wa Mamkala ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kelvya  Gerald Kusaya
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2