WAZIRI wa Maji Mh. Jumaa Aweso amekutana na Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Mwigulu Nchemba kujadili miradi mikubwa ya maji ya kimkakati hususani mradi wa Maji wa Same- Mwanga.
Mawaziri hao kwa pamoja wamekubaliana kushirikiania kuukwamua mradi huo haraka na kumaliza changamoto zote zilizokuwa zimebaki katika utekelezaji wake.
Pamoja na mambo mengine, wameweka mikakati imara itakayozifanya wizara hizo mbili kufanya kazi kwa pamoja sanjari na Wizara ya Mambo ya Nje ili kurahisisha mahusiano na mawasiliano yatakayoleta ufanisi kwenye utekelezaji wa miradi mikubwa ya maji inayohusisha ufadhili.
Kikao hicho kimeudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania nchini Kuwait Mhandisi Aisha S. Amour ambapo nchi ya Kuwait ni sehemu ya wafadhili wakubwa wa mradi huu.
Aidha, baada ya kikao hicho, Waziri Aweso amedhamiria kufika mkoani Kilimanjaro kesho Jumatatu Julai 12, kukutana na uongozi wa mkoa na kuwapa taarifa juu ya hatua zilizofikiwa na serikali katika utekelezaji ya mradi wa Same-Mwanga-Korogwe sanjari na malipo ya wafanyakazi wanaodai stahiki zao.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment