BENKI YA NMB YAJA NA UTARATIBU MPYA WA KUWEKA AKIBA ‘SPEND‌ ‌2‌ ‌SAVE’‌ | Tarimo Blog

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Bw. Filbert Mponzi (kushoto) pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa, Aloyse Maro (kulia) wakizindua rasmi bidhaa mpya ya Benki ya NMB ‘SPEND 2 SAVE’ ambapo mteja aliyejiunga atanufaika na faida kadri anavyofanya matumizi yake. Wengine katikati wakishuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja , Abella Tarimo (pili kushoto) na Mameneja Wandamizi wa benki hiyo, Beatrice Mwambije na Ally Ngingite.

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Bw. Filbert Mponzi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye hafla ya uzinduzi wa bidhaa mpya ya Benki ya NMB ‘SPEND 2 SAVE’ katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya benki hiyo Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa, Aloyse Maro pamoja na Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB, Ally Ngingite. Katika huduma hiyo mteja aliyejiunga atanufaika na faida kadri anavyofanya matumizi yake.
…………………………………………………………………….. ‌‌

Benki‌ ‌ya‌ ‌NMB‌ ‌imekuwa‌ ‌ya‌ ‌kwanza‌ ‌nchini‌ ‌kumuwezesha‌ ‌mteja‌ ‌kuweka‌ ‌akiba‌ ‌kila‌ ‌anapofanya‌ ‌miamala‌ ‌kwa‌ ‌kuzindua‌ ‌huduma‌ ‌maalum‌ ‌kwa‌ ‌ajili‌ ‌hiyo‌ ‌inayojulikana‌ ‌kama‌ ‌“Spend‌ ‌to‌ ‌Save‌ ‌–‌ ‌Miamala‌ ‌Yako‌ ‌ni‌ ‌Akiba‌ ‌Yako”‌ ‌ kupitia‌ ‌waleti‌ ‌maalum.‌ ‌

Huduma‌ ‌hiyo‌ ‌mpya‌ ‌na‌ ‌ya‌ ‌kipekee‌ ‌ni‌ ‌kwa‌ ‌ajili‌ ‌ya‌ ‌akaunti‌ ‌binafsi,‌ ‌akaunti‌ ‌za‌ ‌Chap‌ ‌Chap‌ ‌na‌ ‌akaunti‌ ‌za‌ ‌Mwanachuo.‌ ‌Kuanzishwa‌ ‌kwa‌ ‌huduma‌ ‌hii‌ ‌na‌ ‌NMB‌ ‌ni‌ ‌mapinduzi‌ ‌makubwa‌ ‌ya‌ ‌jinsi‌ ‌ya‌ ‌kuweka‌ ‌akiba‌ ‌na‌ ‌kuwahamasisha‌ ‌ Watanzania‌ ‌kutunza‌ ‌fedha‌ ‌kwa‌ ‌ajili‌ ‌ya‌ ‌matumizi‌ ‌ya‌ ‌baadae‌ ‌na‌ ‌kufanya‌ ‌uwekezaji.‌ ‌

Afisa‌ ‌Mkuu‌ ‌wa‌ ‌Wateja‌ ‌Binafsi‌ ‌na‌ ‌Biashara,‌ ‌Bw.‌ ‌Filbert‌ ‌Mponzi,‌ ‌alisema‌ ‌“Spend‌ ‌to‌ ‌Save”‌ ‌pia‌inadhihirisha‌ ‌ubunifu‌ ‌wa‌ ‌hali‌ ‌ya‌ ‌juu‌ ‌wa‌ ‌NMB‌ ‌wa‌ ‌kuanzisha‌ ‌suluhishi‌ ‌wezeshi‌ ‌za‌ ‌kibenki.‌ ‌Alisema‌ ‌pia‌ ‌ni‌ ‌udhibitisho‌ ‌tosha‌ ‌wa‌ ‌kuwa‌ ‌kinara‌ ‌wa‌ ‌kuwahudumia‌ ‌Watanzania‌ ‌na‌ ‌kuwa‌ ‌mtari‌ ‌wa‌ ‌mbele‌ ‌kuwahamasisha‌ ‌kujenga‌ ‌utamaduni‌ ‌wa‌ ‌ kuweka‌ ‌akiba.‌ ‌

Naye‌ ‌Mkuu‌ ‌wa‌ ‌Idara‌ ‌ya‌ ‌Bidhaa,‌ ‌Bw‌ ‌Aloyse‌ ‌Maro,‌ ‌alisema‌ ‌huduma‌ ‌hiyo‌ ‌mpya‌ ‌pia‌ ‌inaongeza‌ ‌namna‌ ‌bora‌ ‌ya‌ ‌kuwahudumia‌ ‌wateja‌ ‌na‌ ‌njia‌ ‌mojawapo‌ ‌ya‌ ‌kuwakumbusha‌ ‌Watanzania‌ ‌na‌ ‌wateja‌ ‌wa‌ ‌NMB‌ ‌kujitunzia‌ ‌akiba‌ ‌kwa‌ ‌ maisha‌ ‌ya‌ ‌baadae.‌ ‌

Huduma‌ ‌hii‌ ‌ni‌ ‌ya‌ ‌kwanza‌ ‌na‌ ‌ya‌ ‌aina‌ ‌yake‌ ‌kuwahi‌ ‌kutokea‌ ‌nchini‌ ‌Tanzania‌ ‌ambapo‌ ‌mteja‌ ‌anajitunzia‌ ‌fedha‌ ‌zake‌ ‌kupitia‌ ‌miamala‌ ‌yake‌ ‌anayoifanya‌ ‌iwe‌ ‌kununua‌ ‌kitu,‌ ‌kutoa‌ ‌fedha‌ ‌kutoka‌ ‌kwenye‌ ‌akaunti‌ ‌yake‌ ‌au‌ ‌hata‌ ‌kutuma‌ ‌fedha.‌ ‌Huduma‌ ‌ya‌ ‌“Spend‌ ‌and‌ ‌Save”‌ ‌inapatikana‌ ‌kwa‌ ‌mteja‌ ‌kujisajili‌ ‌kupitia‌ ‌zaidi‌ ‌ya‌ ‌ATM‌ ‌8,000‌ ‌za‌ ‌NMB‌ ‌zilizotapakaa‌ ‌nchi‌ ‌nzima‌ ‌na‌ ‌kuweka‌ ‌malengo‌ ‌kwa‌ ‌asilimia‌ ‌ya‌ ‌kila‌ ‌muamala‌ ‌anaoufanya‌ ‌na‌ ‌kiasi‌ ‌kitakachokatwa‌ ‌kwa‌ ‌ajili‌ ‌ya‌ ‌akiba‌ ‌ni‌ ‌kati‌ ‌ya‌ ‌asilimia‌ ‌mbili‌ ‌hadi‌ ‌kumi‌ ‌ya‌ ‌kila‌ ‌muamala‌ ‌utakaofanyika- ‌miamala‌ ‌itakayohusika‌ ‌ni‌ ‌ile‌ ‌inayofanywa‌ ‌kupitia‌ ‌‌ATM,‌ ‌POS,‌ ‌NMB‌ ‌Direct‌ ‌au‌ ‌NMB‌ ‌Mkononi.‌ ‌

NMB‌ ‌imeanzisha‌ ‌utaratibu‌ ‌huu‌ ‌baada‌ ‌ya‌ ‌kugundua‌ ‌kuwa‌ ‌wateja‌ ‌wake‌ ‌wengi‌ ‌hawana‌ ‌tabia‌ ‌ya‌ ‌kuweka‌ ‌akiba‌ ‌na‌ ‌hivyo‌ ‌kuona‌ ‌umuhimu‌ ‌wa‌ ‌kuwaletea‌ ‌huduma‌ ‌ambayo‌ ‌itawasaidia‌ ‌kuweka‌ ‌akiba‌ ‌mara‌ ‌kwa‌ ‌mara‌ ‌na‌ ‌kwa‌ ‌malengo.‌ ‌Aidha,‌ ‌uzuri‌ ‌wa‌ ‌huduma‌ ‌hii‌ ‌ni‌ ‌pia‌ ‌mteja‌ ‌kuweza‌ ‌kutoa‌ ‌fedha‌ ‌zake‌ ‌kutoka‌ ‌kwenye‌ ‌waleti‌ ‌na‌ ‌kuzirudisha‌ ‌kwenye‌ ‌akaunti‌ ‌muda‌ ‌wowote‌ ‌na‌ ‌atakapofanya‌ ‌hivyo‌ ‌ataruhusiwa‌ ‌kutoa‌ ‌mpaka‌ ‌asilimia‌ ‌50‌ ‌ya‌ ‌fedha‌ ‌iliyohifadhiwa.‌ ‌Pia‌ ‌mteja‌ ‌anaweza‌ ‌kujitoa‌ ‌kwenye‌ ‌wallet‌ ‌na‌ ‌fedha‌ ‌zilizohifadhiwa‌ ‌zitarudishwa‌ ‌kwenye‌ ‌ akaunti‌ ‌mama.‌ ‌ ‌

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2