COSTECH YAWATAKA WATAFITI KUZINGATIA USHAHIDI WA KISAYANSI KWENYE TAFITI WANAZOFANYA | Tarimo Blog

TUME ya Taifa Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imesema watafiti ili waweze kufanya tafiti zenye tija katika sekta mbalimbali ni lazima kuwe na ushahidi wa kisayansi unaozingatia weledi ili waweze kutoa matokeo yaliyokusudiwa.

Ofisa Mtafiti Kiongozi upande wa Afya Dk Khadija Malima ametoa kaui hiyo kwenye warsha ilioandaliwa na Tume hiyo dhidi ya watafiti kutoka sekta ya Afya, Kilimo, Mifugo, Maliasili pamoja na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali jiijini hapa.

Ofisa Mtafiti kiongozi huyo amesema nchi inataka matokeo ya uhakika kwa ajili ya kupangia mipango ya maendeleo ya nchi na kufikia malengo ya dira ya mendeleo ya taifa na siyo tafiti za kukaa kwenye vitabu.

Ameafanua kuwa wabunge ndio watunga Sera hivyo watafiti wana wajibu wa kulisaidia bunge ili liwe na taarifa za uhakika za kuwasaidia wabunge kutunga Sera ambazo zitakuwa na tija kwa nchi mana wanaweza kupata uelewa mpana zaidi juu ya sera mbalimbali au sera zinazotarajia kutungwa lazima watafiti watumie nafasi yao bila ili mambo yaweza kwenda vizuri.

" Tanzania tuna document nzuri lakini hazitekelezeki ,mfano tuna Sera ya vijana nzuri sana lakini haitekelezeki,mimba za utotoni bado
ni changamoto licha ya kuwepo kwa Sera hiyo nzuri ambayo inatuongoza,"alisema Dk Khadija.

Pia aliwashauri watafiti kutumia lugha nyepesi katika tafiti zao wanazozifanya  ili kuwarahisishia wanahabari na watanzania wanaozisoma tafiti hizo kusambaza taarifa hiyo kirahisi kwa jamii.

Dk Khadija ameeleza kuwa sekta ya habari ni muhimu sana katika jamii hivyo watafiti nao wanapaswa kuwatumia wanahabari ili kusaidia kutangaza taarifa za utafiti ambazo wamekuwa wakizifanya katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu na Uendelezaji wa tafiti Dk Bugwesa Katale  amesema, jukumu la COSTECH ni kuhakikisha matokeo ya tafiti mbalimbali zinazofanywa hapa nchini yanatumika katika kutunga Sera na mipango mbalimbali ya maendeleo ya nchi,badala ya kuwekwa kwenye makabati.

Dk Katale ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu na uendelezaji wa Tafiti wa COSTECH ameeleza kuwa kumekuwa na changamoto ya tafiti zinazofanywa na watafiti kuishiwa makabatini kuna badala ya kutumika kwenye kutunga Sera na katika mendeleo kwa ujumla kitendo hicho kinapaswa kuachwa.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maarifa wa COSTECH Dk Philbert Luhunga akitoa mada kuhusu matokeo ya tafiti na mchango wake kwenye maendeleo ya nchi amesema kazi ya matokeo ya utafiti ni kuwezesha nchi kufikia malengo 17 ya maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030.

DK Luhanga amesema serikali inataka matokeo ya utafiti yatumike ili kubadilisha jamii huku akisema changamoto ipo kwa watafiti wenyewe katika utekelezaji wa tafiti wanazozifanya.

"ili kuweza kufanikiwa nchi lazima kutumia matokeo ya utafiti katika kutunga Sera ndio maana wanahimiza matokeo ya utafiti yatumike katika kutunga Sera mipango ya maendeleo katika sheria, taratibu na muongozo,"amesema.

Dk Luhunga amesema kazi ya COSTECH  ni pamoja na kuwaweka watafiti pamoja na kuwaunganisha na watunga sera ili kuwe na muunganiko na kuwezesha matokeo ya watafiti kuwafikia watunga Sera.

Mtafiti Kiongozi upande wa Afya kutoka COSTECH, Dk Khadija Malima akizungumzia suala la watafiti kuhakikisha wanakua na ushahidi wa kisayansi wanapofanya tafiti zao.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2