Bodi ya TANESCO yaridhishwa na miradi ya umeme Njombe,wadai maeneo ya miradi yamekidhi vigezo | Tarimo Blog
Na Amiri Kilagalila,Njombe
KUTOKANA na miradi mikubwa ya kuzalisha umeme hapa nchini kwa kutumia maporomoko ya maji ukiwemo mradi wa umeme wa Julius Nyerere unaoendelea kujengwa,kutajwa kutegemea vyanzo vya maji kwa wingi kutoa wilaya za mkoa wa Njombe hususani wilaya ya Makete.
Mkuu wa wilaya ya Makete Juma sweda amesema wananchi wa wilaya hiyo wanapaswa kutazamwa na kukumbukwa kwa kupelekewa nishati ya uhakika ya umeme kwa kuwa wamekuwa na jitihada kubwa za kutunza vyanzo hivyo hatua inayopelekea kuwa na maji ya uhakika wakati wote yanayoweza kuzalisha nishati hiyo.
Hayo yamebainishwa na mkuu huyo wa wilaya wakati alipoongozana na bodi ya wakurugenzi wa shirika la umeme Tanzania (TANESCO) wilayani humo ili kutembelea na kutambua mahali ambapo unatarajiwa kujengwa mradi wa umeme kwa maporomoka ya maji ya mto Rumakali uliopo tarafa ya Bulongwa zitakapozalishwa megawati 222 mara baada ya kukamilika kwa mradi huo unaotajwa kukamilika kwa miezi 36 baadaya ya hatua za awali zinazoendelea hivi sasa.
“Kuna fedha nyingi zitakazoelekezwa katika eneo hili baada ya mradi kuanza na lazima tuulinde na ninaamini na sisi tutakuwa sehemu ya ujenzi kwa kuwa kutakuwa na fursa nyingi,lakini pia wananchi wetu wanapaswa kupata nishati ya uhakika zaidi”alisema Juma Sweda
Aidha katika ziara ya bodi ya wakurugenzi wa shirika la umeme tanzania TANESCO ya kutembelea miradi ya ruhuji wilayani Njombe na Rumakali wilayani makete msimamizi wa muda wa miradi hiyo mhandisi toto zedekia amesema mradi wa rumakali utakapofanikiwa kujengwa na kukamilika basi umeme wake utaingizwa kwenye gridi ya taifa kwa manufaa ya watanzaia wote huku ukisaidia pia kuuza nishati hiyo nje ya nchi.
“Bwawa hili litakuwa na mita za ujazo wa maji wa milioni 256 na umeme uatasafirishwa kwenda kwenye kituo cha kukuza umeme kwa kuwa nchi yetu inakwenda kuwa nchi ya uchumi wa kati kupitia viwanda kwa hiyo lazima tuwe na umeme wa bei naffuu na uhakikia utakaochangia kukua kwa sekta ya viwanda”alisema Toto Zedekia
Dkt,Alexender Kyaruzi ni mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi TANESCO ambaye baada ya kuzulu katika maporomoko ya maji ya mto rumakali amesema jitihada za wataalamu wa nishati katika kutafuta vyanzo vya maji kwa ajili ya kufua umeme ni kubwa na hivyo zinapaswa kuungwa mkono kupitia miradi hiyo.
Aidha amesema bodi ya TANESCO imeafarijika baada ya kuona maeneo yote mawili ya ujenzi wa miradi ya umeme mkoani Njombe kwa kuwa maeneo hayo yamekidhi vigezo na kwamba anaamimni wananchi wa maeneo hayo watanufaika kwa kiasi kikubwa na miradi hiyo.
“Sehemu zote hizo mbili za kufua umeme bodi tumeziona na tumefarijika kuona kwamba sehemu walizochagua wataalam qwetu zimekidhi vigezo ambavyo tulikuwa navyo na matayarisho yanayoendelea tumeona yanakwenda kama ilivyopangwa”alisema Dkt,Alexender Kyaruzi
Juma Kyando na Christon Mahenge ni baadhi ya wakazi wa wilaya ya makete ambao wanasema endapo mradi wa umeme wa rumakali utatekelezwa basi watanufaika pakubwa ikiwemo kupatiwa umeme wa uhakika.
Bodi hiyo imekamilisha ziara yake mkoani Njombe kwa kutembelea miradi miwili muhimu ya kufua umeme kwa kutumia maporomoka ya maji ya mto Ruhudji pamoja na Rumakali iliyopo katika mkoa wa Njombe.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment