Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Kipanga Juma Omary pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Dkt. Amos Nungu wakimsikiliza mmoja wa wabunifu waliopo chini ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH ) mara baada ya kutembelea banda la Tume hiyo katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH ) Dkt. Amos Nungu kutembelea banda la Tume hiyo katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Kipanga Juma Omary pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Dkt. Amos Nungu wakimsikiliza mmoja wa wabunifu waliopo chini ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH ) mara baada ya kutembelea banda la Tume hiyo katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
TAASISI za Elimu nchini ikiwemo COSTECH zimekuwa na ubunifu unaolenga moja kwa moja kutatua changamoto katika jamii.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ameyasema hayo leo Julai 5,2021 alipotembelea banda la COSTECH katika maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Amesema COSTECH imekuwa ikiendeleza wabunifu kila mwaka kwani kumekuwa na mashindano ya Maksatu na wale washindi wamekuwa wakiendelezwa.
"Nimefurahi kuona kwamba zile nadharia ambazo zinafundishwa zinaenda mbali wanaweza kufanya vitu kwa vitendo ambavyo moja kwa moja vinaenda kugusa katika kujenga ujuzi unaomwezesha mtu kujiajiri au kuajiriwa katika sekta ambazo zinagusa changamoto za Watanzania". Amesema Prof.Ndalichako.
Aidha Prof.Ndalichako ametoa wito kwa wabunifu hasa wale ubunifu wao umefika mbali kuwasiliana na COSTECH kupitia mitandao ya kijamii ama kufika katika ofisi zao ili ubunifu wao utambuliwe na kuweza kusaidiwa kupitia kambi za atamizi ambazo ziko COSTECH.
"Katika ubunifu nyingi ambazo nimeziona zinalenga katika kutatua matatizo ya kijamii kwahiyo nitoe wito kama kuna changamoto ya kimasoko pia nalo tutashirikaiana na Wizara ya Viwanda na Biashara tuone ni namna gani tunaweza kuwasaidia kuwatangaza zaidi ili waweze kupata wateja wengi na biashara zao au ubunifu wao uweze kwenda kutoa mchango kwenye taifa letu". Amesema Prof.Ndalichako.
Aidha COSTECH imekuwa mshindi wa pili katika maonesho ya mwaka huu.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment