Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Bi. Shamim Mdee akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango kupata huduma kuhusu mitiani ya kitaalamu ya ununuzi na usajili wa wataalam, wakati wa Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), jijini Dar es Salaam.
Afisa Mwandamizi wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa UTT- Amis Bi. Martha Mashiku, akitoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma za kuwekeza kwa kununua vipande, katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), jijini Dar es Salaam.
Mhasibu wa Kitengo cha Pensheni wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Happiness Mdimidimi akifafanua kuhusu taarifa muhimu zinazohitajika kwa mstaafu ili aweze kupata Pensheni yake kwa wakati, wakati wa Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), jijini Dar es Salaam. Kulia niAfisa Hesabu wa Kitengo hicho Bi. Afiswa Shubi.
Wananchi wakipata elimu ya kozi zinazotolewa katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bw. Emmanuel Ghula (kushoto), akitoa maelezo kwa Bw. Mniko Simon, kuhusu Maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi kwa Mwaka 2022, katika Banda la Wizara ya Fedha na Mipango wakati wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), jijini Dar es Salaam.
Meneja Mikopo wa Benki ya TPB, Bi. Joanitha Deogratias, akitoa elimu kwa wanafunzi wa Sekondari ya Temboni, jijini Dar es Salaam kuhusu akaunti za Watoto, akaunti za muda maalum na bima, walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es Salaam, wakati wa Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba).
Huduma ya Hati za Mishahara na utatuzi wa changamoto za mishahara zikiendelea kutolewa na wataalamu wa Mifumo ya Fedha, katika Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es Salaam, wakati wa Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba).
Mwanasheria Mwandamizi wa Mamlaka ya Rufaa ya Zabuni za Umma (PPAA), Bi. Agnes Sayi, akitoa elimu kwa wanafunzi wa Sekondari ya Temboni jijini Dar es Salaam, waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es Salaam, wakati wa Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba).
Afisa Tehama Mwandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Stella Kyamba (wa tatu kushoto), akitoa elimu ya Hati za Mishahara kwa Watumishi wa umma, kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), jijini Dar es Salaam.
(Picha na WFM, Dar es Salaam)
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment