Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
NAIBU Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira DAWASA imepiga hatua kubwa katika usimamizi wa miradi ya maji nchini ikiwemo matumizi mazuri ya fedha zinazopatikana katika Mamlaka hiyo kwa kuwekeza kiasi cha Shilingi Bilioni 17.8 katika Miradi wa Maji wa Ruvu Juu mpaka Msoga itakayotatua kero ya Maji kwa Wananchi zaidi ya 122,000 wa maeneo hayo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ziara hiyo, Naibu Waziri, Mhandisi Maryprisca Mahundi amewapongeza DAWASA kwa kujituma kutekeleza Miradi hiyo ya kimkakati ili kutatua kero ya Maji katika sehemu mbalimbali za mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Pia amepongeza Watumishi, Wasimamizi wa Miradi yote ya DAWASA wakiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Cyprian Luhemeja katika kufanikisha utekelezaji wa Miradi hiyo takribani 27 sehemu mbalimbali ya Dar es Salaam na Pwani.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Miundombinu na Uwekezaji DAWASA, Mhandisi Ramadhani Mketo amesema Mradi wa Maji wa Ruvu Juu hadi Mboga ni Mradi utakaosaidia kuondoa kero ya Maji katika maeneo ya Mlandizi, Chalinze na Mji Mdogo wa Mboga, pia Mradi huu wanalaza mabomba kwa umbali wa Kilometa 59 katika Mitambo ya Ruvu Juu hadi Chalinze, Mji wa Mboga.
Amesema pia mradi huo utatatua kero ya Maji katika Bandari Kavu ya Kwara na kwenye Mradi wa Reli ya Kisasa ya SGR Kwara, amesema Lita 9,300,000 za Maji zitatumika kwa siku baada ya kukamilika Mradi huo.
Naye, Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mhe. Ridhwan Kikwete amesema ujio wa Naibu Waziri wa Maji katika Maeneo hayo itasidia katika utekelezaji wa Miradi hiyo ya Maji na kuondoa kero kwa Wananchi wake.
Mkurugenzi wa Miundombinu na Uwekezaji DAWASA Mhandisi Ramadhani Mketo akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi kuhusu ulazaji wa Bomba za inchi 10 zinazolazwa kutoka Ruvu Juu mpaka Mboga yenye kilometa 58.9 kwenye Mradi wa Chalinze- Mboga unaotekelezwa na DAWASA. Wa kwanza kushoto ni Msimamizi wa Mradi wa DAWASA, Mhandisi Ishmael Kakwezi
Muonekano wa Bomba la inchi 16 linalolazwa kutoka Ruvu Juu mpaka Mboga litakalokuwa na kilometa 58.9
Kazi ikiendelea
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa Mradi wa DAWASA, Mhandisi Ishmael Kakwezi kuhusu ulazaji wa Bomba unavyopita kwenye ramani kuanzia Ruvu Juu mpaka Mboga kilichopo Wilaya ya Bagamoyo wakati wa Ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na DAWASA.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akikagua mradi wa ulazaji wa mabomba ya inchi 16 katika eneo la Kitongoji cha Mbala kilichopo Kijiji cha Chamakweza wakati wa Ziara yake ya kukagua Miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA.
Kazi ikiendelea
Msimamizi wa Mradi wa DAWASA, Mhandisi Ishmael Kakwezi akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi pamoja na Mbunge wa Chalinze Riziwani Kikwete kuhusu mradi wa kujenga pampu ya kusukuma maji katika Kijiji cha Chamakweza wakati wa Ziara ya naibu Waziri wa maji alipotembelea miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA.
Msimamizi wa Mradi wa DAWASA, Mhandisi Ishmael Kakwezi akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi pamoja na Mbunge wa Chalinze Riziwani Kikwete kuhusu ujenzi wa pampu ya maji ya Msoga wakati wa Ziara ya Naibu Waziri wa Maji.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akiendelea na Ziara yake ya kutembelea miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la ujenzi wa pampu ya maji ya Msoga kuhusu kuridhishwa na miradi inayotekelezwa na DAWASA wakati wa Ziara yake ya kukagua miradi ya maji inayotekelezwa na Mamlaka hiyo.
Mkurugenzi wa Miundombinu na Uwekezaji DAWASA Mhandisi Ramadhani Mketo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa miradi inayosimamiwa na DAWASA wakati wa Ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna wanavyosimamia miradi hasa ya maji ili kuondoa hadha kwa wakazi wa Chalinze ambao wanachangamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi alipokuwa anatembelea miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment