DKT. TULIA ATOA WITO KWA YOMBO VYA HABARI JUU YA TARIFA ZA HALI YA HEWA | Tarimo Blog

 


Na Karama Kenyunko Michuzi TV 

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amevitaka vyombo vya habari nchini, kutenga muda wa kutosha wa kurusha na kutangaza taarifa za hali ya hewa ili wananchi wazipate kwa wakati na kuzitumia kwa ufani.

Dkt. Tulia ameyasema hayo leo Julai 10,2021 wakati wa ziara yake fupi katika Ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) zilizopo Ubungo jijini Dar es Salaam.

Amesema, taarifa za hali ya hewa ni muhimu sana kwa jamii nzima lakini katika vyombo vya habari hapa nchini, taarifa hizi zmekuwa zikitolewa kwa ujumla na kwa ufupi, kitu ambacho kinaweza kuathiri matumizi yake.

“Nitoe wito kwa vyombo vya habari kuangalia namna ambavyo watakuwa wanazitumia taarifa kutoka TMA na kuzitoa mara kwa mara ili kutusaidia sisi wananchi kujiandaa na kufanya maamuzi sahihi katika mipango yetu, tuangalie kama vyombo vingine vya habari vya mataifa ya nje, ukifungua kila wakati unaangalia hali ya hewa” Amesema Dkt. Tulia

Pia Dkt. Tulia ametoa wito kwa wananchi kuitembelea Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ili kujifunza masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na namna taarifa za hali ya hewa zinavyochakatwa kitaalamu hadi kumfikia mtumiaji. 
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania Mhe. Tulia Ackson akipata maelezo ya namna uchambuzi wa hali ya hewa unavyofanyika kwa njia ya modeli za kimahesabu kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi wakati alipotembelea ofisi za TMA, Kituo Kikuu cha Utabiri, Ubungo Plaza, Dar es Salaam.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania Mhe. Tulia Ackson akijionea hindi utabiri wa hali ua hewa kila siku unavyorekodiwa katika studio za TMA kwa ajili ya kuruka katika vyombo mbalimbali vya habari nchini wakati alipotembelea ofisi za TMA, Kituo Kikuu cha Utabiri, Ubungo Plaza, Dar es Salaam.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania, Tulia Ackson akipata maelezo ya namna utabiri wa hali ya hewa unavyoandaliwa kuanzia ngazi za awali kutoka kwa Meneja Kituo Kikuu cha Utabiri, TMA, Samwel Mbuya wakati alipotembelea ofisi za TMA, Kituo Kikuu cha Utabiri, Ubungo Plaza, Dar es Salaam.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania Mhe. Tulia Ackson akipata maelezo ya namna taarifa za hali ya hewa za muda mrefu zinavyohifadhiwa kwa ajili ya matumizi ya sekta mbalimbali ikiwemo miradi ya kimkakati  kutoka kwa Meneja wa Klimatolojia, TMA, Dkt. Hashim Ng'ongolo wakati alipotembelea ofisi za TMA, Makao Makuu, Ubungo Plaza, Dar es Salaam.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2