GCLA kufanya uchunguzi kwa kwa waliozaliwa na jinsia mbili | Tarimo Blog


*Wanaangalia jinsia gani inafanya kazi kwa ufanisi na nyingine kutolewa na madaktari

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV.

 Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) imesema kuwa kwa kushirikiana na madaktari mbalimbali nchini inafanya uchunguzi kwa watoto wanaozaliwa na jinsi mbili tofauti kwa kuangalia ipi inanguvu na inaweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Hayo ameyasema Julai 6, 2021 na Mkurugenzi wa Huduma na Udhibiti anayesimamia Uingizaji, Usambazaji na Matumizi ya Kemikali nchini kutoka Mamlaka hiyo, Daniel Ndiyo katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika viwanja vya Julius Nyerere Sabasaba.

Amesema watoto wanaozaliwa na jinsi mbili tofauti wapo ingawa wanafichwa hivyo mamlaka inaiomba jamii kuacha kuwaficha na kuwaleta kwenye mamlaka hiyo ili waweze kupimwa na kufanyiwa uchunguzi kitaalam  kutokana na uwezo walionao.

"Kwa sasa hakuna haja ya kuwaficha watoto hao, GCLA   anatoa huduma ambapo kwa kushirikiana na madaktari mbalimbali wanafanya uchunguzi wa kudhibitisha ni jinsia  gani ambayo inatawala kati ya kiume na kike," amesema

Amesema wanapofanya uchunguzi wa kimaabara wanaweza kutambua kwamba mtoto huyo ni mwanamke au ni mwanaume hivyo jinsia ambayo inatawala ambayo haitakiwi kuwepo wanawashauri madaktari kuweza kufanya upasuaji ili kumuweza mtoto huyo atambulike kama ni Mwamme au  mwanamke.

Aidha Ndiyo amesema kuwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) imesema kuwa inafanya pia uchunguzi wa vinasaba kwa wagonjwa wa figo  wakati wa kuhitaji mtu wa kumuwekea figo hiyo.

"Figo haitolewi na mtu tu bali lazima kuangalia vinasaba ambavyo vitaruhusu mtu kutoa figo kwa ajili ya mtu mwingine"amwsemamesema Ndiyo.

Amesema kama mtu ana ndugu mwenye matatizo ya figo na anahitaji kutoa figo kwa mgonjwa ni lazima atapimwa ili kuangalia kama zinahusiana au kuwiana.

"Sisi sasa ndio tunafanya uchunguzi  kudhibitisha kwamba watu hao wawili mgonjwa na mtoaji wa figo, figo zao zinawiana, tukigundua zinawiana tunawashauri madaktari wanaendelea na upasuaji wa upandikizaji wa figo," amesema

Amesema katika masuala hayo ya uchunguzi wa figo wamekuwa wakishirikiana na hospital mbalimbali nchini ikiwemo Hospital ya Taifa ya Muhimbili  (MNH) na Aga Khan.

Hata hivyo amesema mamlaka hiyo inatekeleza sheria ya masuala ya usimamizi na udhibiti wa kemikali mbalimbali zinazotengenezwa na kuingizwa nchini.
 
Aidha amesema lengo kubwa la kushiriki maonesho ya mwaka huu ni kuikumbusha jamii majukumu ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali GCLA na shughuli wanazozifanya.

"Majukumu yetu ni mengi ambayo tutawaeleza wananchi lakini tunayomajukumu manne tunayoyafanya ambapo la kwanza ni uchunguzi wa kimaabara wa sampuli mbalimbali ambazo zinafanyika katika maeneo mawili moja ni za jinai na kijamii," amesema

Amesema sampuli za jinai ni pamoja na masuala yanayohusiana na ubakaji, wizi, dawa za kulevya, sumu na sampuli za kijamii ni kuthibitisha ubora wa maji mara baada ya kuchimba kisima cha maji ikiwa ni pamoja pale mtu amekula Chakula na kuleta madhara wanachukua na kufanya uchunguzi wa kubaini ni sumu gani iko kwenye Chakula.

Mkurugenzi wa Huduma na Udhibiti anayesimamia Uingizaji, Usambazaji na Matumizi ya Kemikali nchini kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) Daniel Ndiyo akizungumza na waandishi Habari kuhusiana kazi wanazofanya katika mamlaka hiyo wakati Maonesho ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.


Wananchi wakipata huduma katika Banda Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) katika maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2