*Wabainisha namna nchi itavyonufaika na uwekezaji katika sketa hiyo.
Na Chalila Kibuda ,Michuzi TV Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli(PURA),imesema kuwa hadi sasa Mamlaka yao imeingia mikataba takribani ya Kampuni 11 kati ya hizo ni Kampuni Tatu zipo katika uzalishaji wa mafuta na gesi asilia.
Akizungumza jana mkoani Dar es Salaam,katika maonesho ya 45 ya biashara ya kimataifa sabasaba, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Mhandisi Charles Sangweni
amesema mwaka 2010,PURA ilifikia hadi kampuni 27 lakini ilipofika mwaka 2014 bei ya mafuta ilishuka sana huku kampuni nyingi ziliondoka.
Sangweni amesema katika kampuni hizo 11ni kampuni moja ni la wazawa wa ya kitanzania ambao yanawekeza katika uzalishaji wa sekta hiyo ya mafuta na gesi asilia.
Amesema kila mkataba unaoingia na PURA,ni lazima TPDC iipitie kwani ni mbia hivyo uzawa wao unadhibitisha kupitia TPDC,
"Pamoja na hayo tunachokifanya kwetu , Makampuni yaliyopo katika mikataba sio watekelezaji wa shughuli zote za utafutaji wa mafuta na gesi asilia kwahiyo zipo kampuni nyingine zinazoshiriki kuchimba kwenye kulisha wachimbaji,Ulinzi,Usafiri,Mawasiliano na hayo yote ni Kampuni za kitanzania,"amesema Sangweni.
Amesema fursa zilizopo katika tasnia hiyo ya Mkondo wa juu zinasimamia kupitia sheria ,Miongozo na kanuni, lakini vyote hivyo havitoshi katika usimamizi hadi kuonana na watu wanaosimamia na shughuli hizo ili kuwapa maelezo ya kina juu ya shughuli wanazozifanya na Mamlaka hiyo.
"Kupitia maonesho haya tutawapa maelezo mazuri namna gani anaweza akaja na akatuona au kuingia katika mitandao yetu ili ajue fursa gani ambazo anaweza wakachukua,"alisema na kuongeza
"Hapa nchini kuna rasiliamali nyingi katika shughuli ya utafutaji na mambo mengi hivyo kuna fursa mbalimbali za Ajiira,Chakula,Usafirishaji hivyo hata mtu akiwa mwenyewe anaweza akapata nafasi katika kupata fursa,"alisema
Amesema mwekezaji akiingiza mtaji wake mara baada ya kumaliza na kuanza uzalishaji kinachofuata ni kufanya mgawanyo wa faida na Pura kutokana na kile kilichowekezwa.
Amesema Rasilimali ya mafuta na Gesi asilia lazima zilete faida kwani usimamizi huo ndio utafanya faida kuweza kupatikana.
Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Mhandisi Charles Sangweni wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea Banda la PURA katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato akipata maelezo namna vitu vinavyofanyika katika michoro kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PURA wakati Naibu huyo alipotembelea Banda la Pura katika maonesho ya Sabasaba.Mkuu wa Kitengo cha Ushirikishaji wa Wazawa na Ujumuishaji wa Wadau wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Charles Nyangi akizungumza na waandishi Habari kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo kwenye maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba)jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti ya Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Mhandisi Charles Sangweni akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na kazi ya PURA katika Maonesho ya Sabasaba
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment