AWESO AZITAKA MAMLAKA ZA MAJI KUWA NA UTARATIBU WA KUFANYA TATHMINI | Tarimo Blog

Na Zainab Nyamka, Michuzi TV

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amewataka watendaji wa Mamlaka za Maji safi na usafi wa mazingira nchini kuwa na utaratibu wa kufanya tathmini kila mwaka katika miradi wanayoisimamia.

Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imekuwa mamlaka ya kwanza kuanzisha utaratibu wa kuangalia ya miradi ya maji ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

Waziri Aweso amweza kuzindua cheti cha ubora ISO walichokabidhiwa DAWASA kutokana na ufanisi mzuri wa kazi zao kila siku.

Akizungumza wakati wa hafla iliyofanyika leo, Waziri Aweso amesema Dawasa wamefanya kitu kikubwa sana kwa kuweka wazi mikakati yake ya kuhakikisha wanamtua mama ndoo kichwani kwa kutekeleza Kauli ya Rais Samia Hassan Suluhu kwa vitendo.

Amesema, kabla ya kuunganishwa kwa Dawasa na Dawasco ambazo zilikua ni Mamlaka mbili zinazofanya kazi ya aina moja, Mamlaka hiyo ilikua inaingia mapato ya Bilioni 7 kwa mwaka na upotevu wa maji ukiwa mkubwa sana.

"Hizi mamlaka mmoja alikua anajenga miradi na mwingine anatoa huduma, ila mwaka 2018 tuliamua kuziunganisha na mwaka huu ukiingalia Dawasa inakusanya mapato Bilion 13 kwa mwaka,"amesema Aweso

"Ukiangalia miradi mikubwa ya Kisarawe,Mkuranga, Chalinze Mboga, Kisarawe Pugu imejengwa kwa fedha za ndani kwa kuweka asilimia 35 ya mapato ya kila mwezi tofauti na zamani ambapo walikua wakiomba fedha kutoka serikali,"

Aweso amewapongeza Dawasa baada ya kuzindua magari ya majitaka na vifaa vitakavyotumika katika miradi hiyo ambapo itaenda kuondoa kero ya majitaka kwa wananchi wa Dar es Salaam.

Amesema, Dawasa wametumia Bilion 4.9 kwa ajili ya mradi huo wa majitaka na hata bei elekezi walizoziweka zinamlenga mwananchi wa kipato cha kawaida tofauti na maeneo ya biashara.

Hata hivyo, Aweso amewataka Dawasa kupeleka maji katika maeneo ya nje ya mji kama Chanika Zingiziwa, Mivumoni, Mshikamano,Madale, Wazo na Kibamba ili wananchi wote wapate huduma ya maji safi na salama.

Waziri wa Maji Jumaa Aweso akikata utepe kuashiria kuzindua magari yatakayotumika kuondoa majitaka akishuhudiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Dawasa Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange na Afisa Mtendaji Mkuu Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Nadhifa Kemikimba, mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge na wabunge wa Jiji la Dar es Salaam na Pwani.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2