Waziri Bashungwa Aongoza Kikao cha Kimkakati cha Menejimenti ya Wizara ya Habari Kujadili Bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 | Tarimo Blog

 

 Na. WHUSM – Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa ameongoza kikao cha kimkakati cha Menejimenti ya wizara hiyo kujadili bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/22 mapema hii leo katika Ofisi ndogo za wizara hiyojijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Menejimenti ya Wizara hiyo Waziri Bashungwa amewataka viongozi wa Menejimenti kujadili hoja mbalimbali zilizotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Wakati wa mchakato wa kupitisha ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2021/22.

“Katika kikao hiki cha kimkamkati nataka tuangalie mpango wa utekelezaji wa hoja zilizotolewa Bungeni wakati wa kuwasilisha, kujadili na kupitisha Bungeni bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2021/22,” alisema Waziri Bashungwa.

Nae Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbas amewataka viongozi wa Menejimenti ya wizara kuijadili  bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22 ili kuweza kuitekeleza bajeti hiyo kwa asilimia mia moja.

“Kikao hiki cha Kimkakati cha Menejimenti ya Wizara kina lengo la kupitia bajeti ya mwaka 2021/22 ili kuwa na mkakati wa utekelezaji wa maelekezo ya Viongozi wa Wakuu wa Nchi kwa wizra yetu na maelekezo mbalimbali ya viongozi wa wizara,” alisema Dkt. Abbas.

Katika kikaocha kimkakati  mada mbalimbali zimejadiliwa ikiwa ni pamoja na kukifanya Chuo cha Maendeleo ya Michezo Mallya kuwa Taasisi inayojitegemea pamoja na mkakati wa kubidhaisha lugha ya kiswhili.

Kikao cha Kimkakati cha Menejimenti ya Wizara kimewakutanisha Wakurugenzi wa Idara za Wizara pamoja na Watendaji wakuu wa Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa (wa pili kushoto) akisisitiza jambo kwa Menejimenti ya wizara hiyo (hawapo pichani) wakati wa kikao cha kimkakati kujadili utekelezaji wa bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 mapema hii leo katika Ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam, kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbas, kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt.Ally Possi na wa pili kulia ni Naibu Waziri wa wizara hiyo Pauline Gekul.

Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul (wa pili kulia) akizungumza na Menejimenti ya wizara hiyo (hawapo pichani) wakati wa kikao cha kimkakati kujadili utekelezaji wa bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 mapema hii leo katika Ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam, kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt.Ally Possi na kushoto Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbas na wapili kushoto ni Waziri wa wizara hiyo Innocent Bashungwa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbas (kushoto) akifafanua jambo kwa Menejimenti ya wizara hiyo (hawapo pichani) wakati wa kikao cha kimkakati kujadili utekelezaji wa bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 mapema hii leo katika Ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam, wapili kushoto ni Waziri wa wizara hiyo Innocent Bashungwa, kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt.Ally Possi na wa pili kulia ni Naibu Waziri wa wizara hiyo Pauline Gekul.

Viongozi wa Menejimenti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiendelea na kikao cha kimkakati kujadili utekelezaji wa bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 mapema hii leo katika Ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya viongozi wa Menejimenti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakimsikiliza Waziri wa wizara hiyo Innocent Bashungwa (hayupo pichani) Wakati wa kikao cha kimkakati kujadili utekelezaji wa bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 mapema hii leo katika Ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam.Picha na WHUSM –Dar es Salaam




Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2