KATIBU MKUU MASSAWE AAGIZA MRADI WA BABATI UKAMILIKE NDANI YA MWEZI MMOJA | Tarimo Blog

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Andrew Wilson Massawe ametembelea na kukagua hatua za mwisho za ujenzi wa Mradi wa Kuongeza Uwezo wa Kuhifadhi Nafaka (Storage Capacity Expansion Project) katika eneo la Babati.

Ujenzi wa mradi huo unatekelezwa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA chini ya Mkandarasi UNIA SP Z O O Kutoka Nchini Poland.

Mradi huo ukikamilika utakuwa na uwezo wa kuhifadhi tani elfu arobaini (40,000).

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu Kilimo aliongozana na Afisa Mtendaji Mkuu wa NFRA, Milton Lupa pamoja na baadhi ya wajumbe wa menejimenti ya wakala hiyo.

Mradi huo wa eneo la Babati mpaka sasa umefikia asilimia 99.8 na Katibu Mkuu amefurahishwa na kazi nzuri iliyofanyika na hatua ambayo mradi umefikia.

Aidha ameilekeza Menejimenti ya NFRA kuhakikisha mkandarasi anamalizia kazi zilizobaki ndani ya mwezi mmoja ili Vihenge na Maghala hayo yaweze kuanza kutumika.

Katibu Mkuu Wa Wizara ya Kilimo Andrew Massawe akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA baada ya kutembelea mradi wa kuongeza uwezo  wa kuhifadhi chakula uliopo Babati Mkoa wa Manyara
Katibu Mkuu Wa Wizara ya Kilimo Andrew Massawe akipata maelezo kuhusu mradi wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi chakula (storage capacity Expansion Project) kutoka Mhandisi Immani Nzobo. Waliosimama nyuma ni  Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA Milton Lupa na pembeni ni Mkurugenzi wa Masoko Mikalu Mapunda
Katibu Mkuu Wa Wizara ya Kilimo Andrew Massawe akipata maelezo kuhusu mradi wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi chakula (storage capacity Expansion Project) kutoka Mhandisi Immani Nzobo (kulia), Katibu Mkuu alitembelea mradi huo ambao umefikia aslimia 99.8 ukiwa na uwezo wa kuhifadhi tani elfu arobaini (40,000)
 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2