LHRC YAJA NA MPANGO WA KULINDA HAKI ZA MAKUNDI MAALUMU. | Tarimo Blog

Na Farida Saidy Morogoro.

Katika kuendelea kutokomeza vitendo vya ukatili katika jamii , Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimesema kimeandaa mpango maalumu wa kulinda na kutetea haki za makundi maalumu wakiwemo wanawake, watoto na watu wenye ulemavu.

Akizungumza kwenye kikao  kazi cha kupitia ubora wa mabaraza ya ndoa na sheria za uasili watoto kilichofanyika mkoani Morogoro,  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Wakili Anna Henga amesema matatizo ya ndoa yamekuwa ni changamoto katika jamii na kupelekea wanawake kuishia kubaki na watoto Jambo linalosababisha kuongeza kwa watoto wa mitaani.

"Watoto huathiriwa zaidi na migogoro ya ndoa kwani wengi hutelekezwa na huingia katika wimbi la vitendo vya kikatili hasa pale familia zinapovunjika na watoto wengi hukosa muongozo, hivyo idadi ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani inaongezeka",amesema Anna Henga.

Aidha Henga ameongeza kuwa kituo Cha Sheria na Haki za Binaadamu kimeandaa mipango mikakati mitano ikiwemo mpango mkakati wa kulinda na kutete Haki za makundi maalumu wakiwemo wanawake.watoto na watu wenye Ulemavu.

Ameongeza kuwa ripoti ya Haki za Binaadamu ya Mwaka 2020 inayoandaliwa na kituo Cha Sheria na Haki za Binaadamu imerupoti zaidi ya kesi 26,544 za ukatili kwa Wanawake ikiwemo vifo 32 vya wanawake kuuawa na wenza wao.

Kwa upande wake Twaha Kibarula ambaye ni  Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto amesema kikao hicho kitajalidi na kuweka utaratibu bora utakaowasaidia watoaji huduma za usuluhishi wa migogoro ya ndoa kutoka ngazi mbalimbali.

"Hapa tutajadili njia bora zaidi ya wazazi au walezi kupata vibali kisheria ili waweze kupata huduma za malezi ya kambo na kuwasili kwa kiingereza tunaita fostcare and adoption, kutokana na utendaji wa jambo hili ulikuwa hauko sawa", amesema twaha.


 
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2