Mwenyekiti wa Tanzania Peace Foundation (TPF) taifa, Sadiki Godigodi kulia akimkabidhi Mganga mfawidhi wa hospitali ya vijibweni, Daktari Mtiba Nyagucho mara baada ya kuchangia damu katika hospitali ya Vijibweni Kigamboni jijini Dar es Salaam.
TAASISI ya Tanzania Peace Foundation (TPF) wafanya usafi, wajitolea damu na wata msaada wa vitu mbalimbali katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala pamoja na hospitali ya Mkoa ya vijibweni iliyopo wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Hospitali zilizotembelewa na wanachama wa Tanzania Peace Foundation ni Mwananyamala, Vijibweni Kigamboni, Amana pamoja na Temeke hospitali.
Akizungumza katika hospitali ya Mkoa ya vijibweni iliyopo wilaya ya Kigamboni Mwenyekiti wa Tanzania Peace Foundation (TPF) taifa, Sadiki Godigodi amesema kuwa kutokana na taasisi hiyo kujihusisha na masuala ya amani hapa nchini wameona kuwa changamoto nyingi katika afya ndio maana wameanza kwa kutoa msaada pamoja na kujitolea damu katika hospitali zilizopo jiji la Dar es Salaam.
"Amani ni neno mtambuka kwani lipo maendeo mengi ndugu zetu ambao wapo hospitali wanachangamoto nyingi na tukumbuke kuwa sisi ni wagonjwa watarajiwa, lakini kunamahitaji mhimu ili huyu mgonjwa awe na amani lazima awe na afya njema, kama afya imeteteleza mgonjw hawezi kuwa na amani na furaha."
Godi godi amesema kuwa uchangiaji wa damu ambao umefanywa na wanapeace foundation utaenda kuimarisha afya za wagonjwa kadhaa ambao walikuwa na upungufu wa damu nao watakuwa na amani.
Hata hivyo Godigodi amewaimiza watanzania wengine kuiga mfano wa taasisi ya Tanzania Peace Foundation ili kuweza kuokoa maisha ya watu wengi zaidi wenye uhitaji wa damu.
Damu hii itamsaidia dada, mama, baba, kaka na mtoto kwahiyo utakuwa umeokoa maisha ya mwezako na maisha ya nduguyako leo unaweza kuwa umelazwa wewe na ukawa na uhitaji wa damu kile kitendo ulichokifanya kitakuja kukulipa baadae, lakini si hivyo tuu hii ni baraka kubwa sana kutoka kwa Mungu.
Kwa upande wa Mganga mfawidhi wa hospitali ya vijibweni, Daktari Mtiba Nyagucho amewashukuru Taasisi ya Peace Foundation kwa kuona hitaji la hospitali ya vijibweni na kuiweka hospitali hiyo katika rekodi ya hospitali zanye mahitaji na kuamua kufika na kutoa msaada katika hospitali hiyo.
Hata hivyo Dkt. Mtiba ameomba wadau wengine kuchangia mashuka kwahi hospitali hiyo inauhaba wa mashuka ya kutandika katika vitanda vya wagonjwa wanapolazwa katika hospitali hiyo.
Nae Mwenyekiti wa Tanzania Peace Foundation wilaya ya Kinondoni, Abdalha Hamadi walipowasili katika hospitali ya Mwananyamala amesema kuwa lengo la kufika katika hospitali ya hiyo ni kutoa msaada wa vitu mbalimbali, kufanya usafi katika mazingira ya hospitali pamoja kuchangia damu ikiwa ni njia mojawapo ya kusambaza amani kwa watu wote hap nchini.
Amewaomba wadau wengine wa maendeleo hapa nchini kusaidia kwa hali na mali hospitali zetu na sio kuiachia serikali peke yake. "Hata sisi tunamajukumu na umhimu wa kusaidi kila mmoja kwa nafasi yake ili mambo yaende." Amesema Mwenyekiti Hamadi
Hivyo Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto, Irene Balongo akizungumza katika hospitali ya Mwananyamala leo Julai 23,2021 amesema kuwa changamoto kubwa katika hospitali hiyo ipo kwa wanawake wanaojifungua kwani wengi wanaofariki dunia ni wale waopoteza damu nyingi wakati wa kujifungua. "Hivyo tunawashukuru sana wanachama wa Tanzania Peace Foundation kwa kuchangia damu katika hospitali hii ya Mwananyamala itawezesha kuokoa maisha ya watu wengine, tunahitaji damu sana kwaajili ya afya za kinamama." Amesema Dkt. Irene
Hata hivyo mwakilishi wa wanawake waliopata msaada huo, Lina Woiso amewashukuru wanataasisi ya Peace Foundation kwa kutoa msaada huo. Tunawashukuru mnapokuja hivi tunapata moyo, mnatupa maneno ya faraja kwahiyo wale waoaweza kusaidi waendelee kuwakumbuka wagonjwa waliopo hospitalini." Amesema Lina
Wanachama wa Tanzania Peace Fondation wakiingia katika hospitali ya vijibweni Kigamboni jijini Dar es Salaam leo.
Wanachama wa Tanzania Peace Foundation wakiwa katika picha ya pamoja walipotembelea hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo.
Viongozi wa Tanzania Peace Foundation wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakijiandaa kuingia katika wodi ya wanawake waliojifungua katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Tanzania Peace Foundation wilaya ya Kinondoni, Abdalha Hamadi na viongozi wengine wakimkabidhi vifaa mbalimbali vya tiba pamoja na vifaa vya wamama katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo Julai 23,2021.
Wanachama wa Tanzania Peace Foundation wakiwa katika picha ya pamoja walipotembelea hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo.
Viongozi wa Tanzania Peace Foundation wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakijiandaa kuingia katika wodi ya wanawake waliojifungua katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Tanzania Peace Foundation wilaya ya Kinondoni, Abdalha Hamadi na viongozi wengine wakimkabidhi vifaa mbalimbali vya tiba pamoja na vifaa vya wamama katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo Julai 23,2021.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment