NAIBU WAZIRI DKT MABULA AAGIZA WATENDAJI ARDHI KUSHIRIKI ZIARA ZA VIONGOZI | Tarimo Blog

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimjulia hali Mzee Mohamed Kidume mkazi wa Mtwara Mikindani mwenye umri wa miaka 97 katika eneo la Mji wa Kale wakati wa ziara yake mkoani Mtwara. Mzee Kidume ni mmoja wa wazee waliompokea Mwl. Nyerere wakati wa harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi katika mkoa wa Mtwara tarehe 23 Julai 2021 wakati wa ziara ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi mkoani humo.
Sehemu ya Wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi katika mkoa wa Mtwara wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati wa ziara ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Mtwara tarehe 23 Julai 2021.

mkazi wa Mtwara Sheikh Nurdin Abdalah Manguji akiwasilisha kero yake ya ardhi kwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati wa ziara ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi mkoani humo.

 


Na Munir Shemweta, MTWARA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka watendaji wa sekta ya ardhi kushiriki katika ziara za viongozi ili kuweza kujibu changamoto zitakazojitokeza wakati wa ziara.

"Kiongozi akija eneo lako hakikisha uko katika msafara kama suala la ardhi likijotokeza basi wewe uweze kutoa ufafanuzi ili hatua zichukuliwe" alisema Dkt Mabula

Akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi mkoani Mtwara tarehe 23 Julai 2021, Dkt Mabula aliwataka watendaji wa sekta ya ardhi katika mikoa kuhakikisha wanakuwa na daftari maalum la kuorodhesha migogoro ya ardhi na hatua zilizochukuliwa sambamba na kuandika taarifa kuhusiana na migogoro husika kwenda ofisi za wakuu wa wilaya.

"Kumekuwa na utaratibu akija kiongozi mpya migogoro inaibuka upya sasa mhakikishe migogoro hiyo inaandikwa kwenye mfumo wa matrix ili kmrahisishia  kiongozi na kumuepusha kupokea malalamiko yaliyokwisha fanyiwa kazi.

Aidha, katika kuhamasisha wanachi kulipa kodi ya ardhi Dkt Mabula alizitaka halmashauri kuandika taarifa ya jinsi zilivyotoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari kama vile redio za kijamii.

Pia aliwaeleza watendaji wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Mtwara kuwa anafikiria namna ya kuanzisha ushindani wa ukusanyaji kodi ya ardhi katika halmashauri kwa lengo la kuona halmashauri iliyofanya vizuri zaidi.

katika kujenga nidhamu ya watumishi, Dkt Mabula aliagiza watumishi wa sekta ya ardhi kutotoka nje ya vituo vyao vya kazi bila wakurugenzi kuwa na taarifa na kusisitiza kuwa watumishi wa ardhi wanatakiwa kutatua migogoro na si kuwa sehemu ya migogoro.

Akielezea upangaji miji katika maeneo mbalimbali nchini Naibu Waziri wa Ardhi alisema, pamoja na Wizara kusaidia harakati za upangaji Upimaji  na umilikishaji ardhi katika halmashauri lakini jukumu la upangaji linabaki kwa halmashauri kwa kuwa ndiyo mamlaka ya upangaji.

" Si jukumu la wizara kuingilia upangaji wa miji katika halmashauri ila inazisaidia kuzikopesha fedha na kueleza kuwa zipo halmashauri zilizopewa milioni 200 hadi 300 lakini zipo nyingine zimetumia fedha kwa mambo mengine na nasisitiza pesa ziende katika masuala ya ardhi" alisema Dkt Mabula.

Mmoja wa wananchi wa Mtwara Sheikh Nurdin Abdalaah Manguji anayemiliki takriban hekta 8.704 katika eneo la Shangani West Mtwara   aliimuomba serikali kupitia wizara ya Ardhi kumsamehe  kodi anayodaiwa miaka ya nyuma kwa kuwa hakuwahi kufahamishwa na kupatiwa nyaraka za eneo lake.



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2