MHANDISI MASAUNI AIAGIZA PPRA KUDHIBITI RUSHWA KWENYE UNUNUZI WA UMMA. | Tarimo Blog

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mhandisi Hamad Yusuff Masauni (Mb), akizungumza wakati alipotembelea Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), kwa lengo la kufahamiana na kupanga mikakati ya kuboresha utendaji katika Mamlaka hiyo, jijini Dodoma.



Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu na ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kujenga Uwezo na Huduma za Ushauri wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Mhandisi Mary Swai akifafanua majukumu yanayotekelezwa na Mamlaka hiyo wakati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mhandisi Hamad Yusuff Masauni (Mb), alipotembelea Mamlaka hiyo, jijini Dodoma.



Mkurugenzi wa Mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa PPRA, Bw. Peter Shilla, (aliyenyoosha mkono) akitoa ufafanuzi namna ya mfumo wa ununuzi kwa njia ya mtandao unavyotumika wakati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mhandisi Hamad Yusuff Masauni (Mb) alipotembelea Mamlaka hiyo, jijini Dodoma.



Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mhandisi Hamad Yusuff Masauni (Mb), akipokea Kitabu cha Sheria ya Ununuzi wa Umma (2021) na Maboresho yake ya mwaka 2016, kutoka kwa Kaimu Afisa Mtendaji ambaye pia ni Mkuu na Mkurugenzi wa Kujenga Uwezo na Huduma za Ushauri wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Mhandisi Mary Swai, jijini Dodoma.



Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mhandisi Hamad Yusuff Masauni (Mb), akipokea Ripoti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), ya utendaji kazi ya mwaka 2019/20 kutoka kwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kujenga Uwezo na Huduma za Ushauri wa PPRA Mhandisi Mary Swai, jijini Dodoma.

Afisa Mahusiano Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw. Mcharo Mrutu, akizungumza wakati akimkaribisha Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mhandisi Hamad Yusuff Masauni (Mb), alipotembelea ofisi za Mamlaka hiyo, jijini Dodoma.



Baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), wakifuatilia mazungumzo wakati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mhandisi Hamad Yusuff Masauni (Mb), alipotembela ofisi za Mamlaka hiyo, jijini Dodoma.



Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mhandisi Hamad Yusuff Masauni (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), baada ya kikao alipotembela Ofisi za Mamlaka hiyo, jijini Dodoma.



Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), baada ya kikao alipotembela Ofisi za Mamlaka hiyo, jijini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM, Dodoma)

**********************************

Na Saidina Msangi, Dodoma

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Mhandisi Hamad Yusuff Masauni ameiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), kuongeza kasi ya ukaguzi wa masuala ya ununuzi katika taasisi za Umma ili kubaini mapungufu na kuchukua hatua kabla ya kuisababishia Serikali hasara.

Mheshimiwa Masauni ametoa maagizo hayo jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti pamoja na Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo akiwa katika ziara yake ya kutembelea Taasisi zote zilizochini ya Wizara ya Fedha na Mipango.

Alisema kuwa Serikali inatumia kiasi kikubwa cha fedha kwenye ununuzi akitolea mfano Bajeti iliyopita ya Mwaka wa Fedha 2020/2021 ambapo Shilingi trilioni 25 sawa na asilimia 75 ya Bajeti yote zilitengwa kwa ajili ya kufanya ununuzi.

“Ili kudhibiti matumizi yasiyofaa ya fedha za Umma, ni lazima Idara ya ufuatiliaji na Ukidhi ipatiwe wafanyakazi wa kutosha na wenye weledi ili ukaguzi ufanyike kwa ufanisi na kupunguza hasara kwa Taifa” alisema Mhe. Masauni.

Maelekezo ya Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Hamad Yusuff Masauni yanakuja baada ya kuelezwa kuwa kutokana na changamoto ya uhaba wa watumishi katika Idara ya Ufuatiliaji na Ukidhi, PPRA inakagua wastani wa taasisi 120 katika taasisi 540 kwa mwaka.

Aidha, Dkt. Masauni aliipongeza Taasisi hiyo kwa kusimamia Mfumo wa Ununuzi kwa njia ya Mtandao ujulikanao kama TaNEPS lakini akaagiza wataalam wa ndani wauboreshe ili kuhakikisha kuwa haitoi mwanya wa kutoa zabuni kwa watu wasio na vigezo na wanaotumia rushwa.

“Ni muhimu kuhakikisha kuwa mnapunguza uwezekano wa watumishi kukutana na wazabuni ana kwa ana ili kuepusha mazingira yanayoweza kuchochea rushwa na kuisababishia Serikali hasara” alisisitiza Mhe. Masauni.

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi Serikalini (PPRA) Mhandisi Mary Swai, alisema kuwa Mamlaka yake inakabiliwa na upungufu wa watumishi ambapo kwa sasa ina watumishi 76 sawa na asilimia 48.

Alimshukuru Mhandisi Masauni kwa kuwatembelea kujua majukumu yao ya kila siku na kuahidi kuwa maagizo yote aliyowapatia yatafanyiwa kazi kikamilifu na kwamba wataendelea kufanya kazi kwa weledi na ufanisi mkubwa katika kuhakikisha kuwa sekta ya ununuzi wa umma inaleta tija na maslahi kwa Taifa.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2