WAFANYABIASHARA watano jijini Dar es Salaam wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka 14, likiwemo la kuisabishia ya Benki ya NMB hasara ya Sh.Milioni 365
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Ashura Mzava mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Joseph Luambano imewataja washtakiwa hao kuwa ni, Reginald Massawe(38), Gaston Danda(38), Cladius Kabwogi(34), Irene Marwa(25) na Noel Kitundu(34).
Mbali na kusabisha hasara washtakiwa hao ambao wanaishi maeneo tofauti tofauti jijini humo wanakabiliwa na shtaka la kuongoza genge la uhalifu, pia yapo mashtaka nane ya kughushi, lipo shtaka la kujipa utambulisho usio wake na mashtaka matatu ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Imedaiwa kati ya Desemba mwaka 2019 na Novemba mwak 2020, katika jiji la Dar es Salaam, washtakiwa waliongoza genge la uhalifu kwa kughushi, kuiba na kutoa utambulisho usio wa kwake.
Mshtakiwa Massawe na Danda wanadaiwa, Desemba 17, 2019 kwa nia ya kutenda kosa, walighushi maombi ya fomu ya Benki na taarifa za huduma kwa mteja za benki ya ABC. Pia Masawe anadaiwa kughushi leseni ya biashara na cheti cha usajili wa malipo ya kodi kwa nia ya kuonyesha kwamba nyaraka hizo Ni halali na zimetolewa na Shirika la umeme Tanzania (Tanesco) huku wakijua kuwa siyo kweli.
Aidha imedaiwa Desemba 10,mwaka 2019 katika benki ya NMB tawi la Msasani ndani ya Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam alijitambulisha kuwa yeye Riziki Kayenga na anafanya kazi Tanesco na kutumia nyaraka hizo kufungua akaunti yake binafsi huku akijua kuwa siyo kweli.
Katika shtaka la kuwasilisha nyaraka za uongo inadaiwa, Septemba 30, huko Mlimani City, mshtakiwa Masawe kwa makusudi na kwa nia ya kutenda uovu aliwasilisha barua ya utambulisho kutoka Tanesco kwa dhamuni la kuonesha kuwa Riziki Kayenga ni muajiriwa wa shirika hilo na kwamba nyaraka hizo ni za halali wakati siyo kweli.
Aidha inadaiwa washtakiwa hao wakiwa huko katika benki ya NMB eneo la Mlimani, wilayani Ubungo washtakiwa wote kwa njia ya udanganyifu walijipatia mikopo ya zaidi ya sh. Sh. Milioni 190 kwa njia mbali mbali kwa kubadirishana utambulisho wao.
Imeendelea kudaiwa kati ya Desemba mwaka 2019 na Novemba mwaka 2020 jijini Dar es Salaam washtakiwa wote kwa njia ya udanganyifu waliisababishia benki ya NMB hasara ya Sh. Milioni 360.
Washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo na wamerudishwa rumande hadi Julai 15,2021.Juni 29, 2021 Washtakiwa hao walifutiwa kesi ya uhujumu uchumi na mashtaka ya utakatishaji fedha na kisha kuwafungulia kesi ya jinai.
Hata hivyo, leo walipofika mahakamani mahakama iliwafutia kesi hiyo lakini walikamatwa na kisha kufunguliwa kesi ya ujumu uchumi upya
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment