Na Yeremias Ngerangera, Namtumbo
Naibu waziri wa kilimo ushirika na umwagiliaji Husein Bashe aliyasema hayo wakati wa kukagua mashamba ya NAFCO ( National Agriculture and food cooperation ) nyumba za wafanyakazi zilizotelekezwa pamoja na kukagua kituo cha utafiti cha uyole kilichopo kijiji cha suruti wilayani Namtumbo ambacho nacho hakifanyi kazi na kusema kuwa mwache Mwalimu Nyerere aitwe baba wa taifa .
Bashe alionesha kusononeshwa na Juhudi zilizofanywa na mwalimu wakati wa utawala wake wa kutaka kuimarisha kilimo na kuanzisha mashamba ya NAFCO Pamoja na kuanzisha kituo cha utafiti cha mbegu katika kijiji cha Suruti alidai jitihada hizo lazima zienziwe kwa kuhakikisha kituo cha utafiti hicho kinafanya kazi kama kilichokusudiwa pamoja na kuhakikisha mashamba ya NAFCO yanalimwa kama lengo lilivyokusudiwa .
Bashe alikagua Ghala kubwa la NAFCO ,mashamba hekta 6000 kukagua nyumba zilizokuwa zinatumiwa na wafanyakazi ni nyumba 17 huku katika kituo cha utafiti pia alikagua mashamba hekta 388 na nyumba 16 zilizokuwa zinatumiwa na watumishi wa kituo wakati kituo kinafanya kazi.
Matenus Kapinga mwangalizi wa shamba na nyumba za NAFCO alisema kuwa kazi yake kubwa ni kukodisha mashamba na kiasi cha fedha kinachopatikana kinaingizwa katika akaunti ya wizara ya fedha kwa kuwa wizara ya fedha ndiye mmiliki wa mashamba hayo.
Generosa Kayombo mkulima katika mashamba ya NAFCO alifikisha malalamiko ya wakulima kwa Naibu waziri wakilalamikia bei ya pembejeo za mbolea lakini pia wakalalamikia bei ndogo ya mazao ya mkulima akitolea mfano wa zao la mahindi ambalo kwa sasa bei ya soko kilo ni shilingi 220.
Katika ziara hiyo pia Naibu waziri alikagua ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha vifungashio na kusikiliza kero kutoka kwa meneja wa chama kikuu cha ushirika Juma Mwanga ya kutonunuliwa kwa tumbaku tani 200 ambapo pamoja na mambo mengine waziri alikipongeza chama kikuu SONAMCU kwa kutumia mapato yao ya ndani kujenga kiwanda hicho lakini akaahidi kuongea na makampuni yanayonunua tumbaku ili kuimalizia tumbaku tani 200 za wakulima zilizobaki alisema Bashe.
Ziara ya waziri wa kilimo wilayani Namtumbo imetoa majibu kwa viongozi wa wilaya kujibu malalamiko ya wananchi waliokuwa wanahitaji kurejeshewa mashamba ya NAFCO na yale ya chuo cha utafiti Suruti yarudishwe kwa wananchi ili waweze kugawiwa kutokana na mashamba hayo kutelekezwa na kutofanya kazi iliyokusudiwa Bashe amewahakikishia viongozi wa wilaya kuwa serikali kwa sasa itahakikisha mashamba hayo yanafanyakazi kama ilivyokusudiwa kuanzia sasa.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment