Mwenyekiti Umoja wa Vijana Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Taifa, Eng.Aivan Maganza.
MWENYEKITI Umoja wa Vijana Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Taifa, Eng.Aivan Maganza azidi kupigilia msumari kuhusu wanaoomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan Katiba Mpya.
Amesema kuwa kunamakundi 18 yanayoungana katika kutengeneza katiba mpya lakini ni vyama vya Siasa tuu ndio vinavyopigania kupata katiba mpya na sio wananchi kama wao wanavyodai.
Akizungumza leo jijini Mwanza Eng. Maganza amesema kuwa vyama vya siasa ni kundi moja tuu hivyo halitoshi kuwasemea wananchi kuwa wanataka katiba mpya, kwasababu kundi moja halishawishi kupata katiba mpya basi wakashawishi makundi 17 yaliyobaki kwani wao tuu hawatoshi.
Hata hivyo amzidi kusisitiza kuwa vyama vya upinzani nchini kuacha kumchonganisha Rais Samia Suluhu Hassan na wananchi kwa kitendo chao cha kudai katiba mpya ili hali suala hilo halipo katika ilani ya chama cha Mapinduzi (CCM).
Hata hivyo amehoji Chama cha Siasa cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinachodai Katiba Mpya, Rais atapata wapi fungu la fedha za kuanza kujadili Katiba? Ingali bajeti ya 2021/ 2021 hakuna fedha zilizotengwa kwaajili ya katiba mpya.
Hata hivyo Eng. Maganza amesema kuwa kwa sasa vyama vya siasa viachane na dhana ya katiba mpya na waache Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania afanye kazi ya kujenga nchi.
Hata hivyo ameombwa wananchi kujenge nchi kwanza na baadae ikifikia wakati wa katiba tutaitengeneza katiba mpya na mengine baadae.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment