NBAA YAENDELEA KUTOA ELIMU KWENYE MAONESHO YA 45 YA KIMATAIFA YA BIASHARA | Tarimo Blog

 

Afisa Masoko na Mawasiliano wa NBAA, Magreth Kageya akitoa maelezo Kwa maafisa wa TBS kuhusu jinsi ya kujisajili kwa ajili ya kufanya Mitihani, maelekezo kwa juu ya ulipaji wa ada mbalimbali kwenye banda la Bodi hiyo lililopo ndani ya Wizara ya Fedha na Mipango leo katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. 
Afisa kutoka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu(NBAA), Irene Mutagaywa(wa kwanza kushoto) akitoa maelezo kuhusu Usajili wa Wanafunzi ili kuweza kufanya mitihani ya Bodi hiyo kwa ngazi mbalimbali  kuanzia ngazi ya chini (Accounting Technician)  mpaka  ile ya Taaluma (Profession) leo katika banda la Bodi hiyo lililopo ndani ya Wizara ya Fedha na Mipango kwenye Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Afisa Masoko na Mawasiliano wa NBAA, Magreth Kageya akijibu maswali aliyokuwa anaulizwa na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Temboni iliyopo Kimara  Dar es Salaam waliotembelea Banda la Bodi hiyo katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.   

 Afisa kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Edes Ernest akiuliza kww wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu(NBAA) mara walipotembelea Banda la Bodi hiyo lililopo ndani ya jengo la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. 
Wafanyakazi wa Bodi ya NBAA wakeindelea kutoa huduma kwenye banda la Bodi hiyo leo.
 Mchezaji wa zamani wa Yanga na timu ya Taifa (Taifa Stars), Ally Mayai “Tembele”(wa kwanza kulia) akiuliza baadhi ya maswali yanayohusu bodi ya NBAA alipotembelea Banda lao katika  Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. 

Maafisa kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS)wakisaini Kitabu mara baada ya kutembelea Banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu(NBAA) kwenye Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. 
Wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu(NBAA) wakiongozwa na Afisa Masoko na Mawasiliano Magreth Kageya(wa pili kushoto), Hassan Kawambwa(wa kwanza kushoto) Loyrd L. Chiloleti(wa kwanza kulia) pamoja na Irene Mutagaywa(wa pili kulia) kwenye banda la Bodi hiyo lililopo ndani ya Wizara ya Fedha na Mipango. 



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2