UDOM YAJIPANGA KUWAHUDUMIA WANANCHI MAONESHO YA SABASABA, YAFUNGUA DIRISHA LA UDAHILI | Tarimo Blog

  

Mkurugenzi katika Kurugenzi ya Shahada za Juu kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma,  Profesa Frowin Paul Nyoni akitolea ufafanuzi kwa wananchi waliofika kwenye Banda la Udom kuhusu namna ya udahili kwa wanafunzi wapya wa mwaka wa masomo wa 2021/22 kwenye Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. 
Mhadhiri msaidizi Idara ya  Sanaa Bunifu na Taaluma za habari kutoka Chuo kikuu cha Dodoma, Peter Msuya akitoa ufafanuzi kuhusu ubunifu wa sanaa za mikono zilizofanywa na wanafunzi wa UDOM kwa maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania(TBS) waliotembelea Banda la chuo hicho katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. 
Mhadhili Msaidizi Idara ya Kemia  kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma, Miraji Hossein akitolea ufafanuzi kuhusu mtambo wa kusafishia maji uliotengenezwa na chuo hicho kwenye Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. 
Mhadhiri Mwandamizi ambaye ni  Mratibu katika kurugenzi ya Shahada za Juu kutoka UDOM, Dkt. Peter Josephat Kivigiti akisikiliza maswali kutoka kwa mwananchi aliyegifika kwenye Banda la chuo hicho alipokuwa anataka kujua namna gani wanafunzi wanavyoweza kufanya udahili kwa njia ya mtandao katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri kutoka Idara ya Uhandisi wa Mawasiliano, Mkuuwa Idara ya Ubunifu na Ujasiriamali chuo kikuu cha Dodoma, Dkt. Alex Frank Mongi akitoa maelezo kuhusu ubunifu wa teknolojia unaofanywa  na Chuo hicho kwa maafisa wa TBS waliotembelea Banda la chuo hicho.
Mhadhiri Mkuu wa Idara ya Tiba kwa Jamii Shule ya Tiba ya Afya ya kinywa kutoka UDOM, Deogratius Bintabara akifafafanua jambo.
Kazi ikiendelea 
Muonekano wa Mtambo wa kusafisha maji
Muonekano wa banda ka Chuo Kikuu cha Dodoma kwa nje

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2